Mstahiki meya wa jiji la Arusha Kalist Lazaro akiongea wakati akifungua
na kufunga baraza la madiwani la Jiji hilo kwenye kikao cha baraza la
madiwani cha robo ya mwisho ya mwaka 2018\19 kilichofanyika kwenye
ukumbi wa shule ya sekondari Arusha jijini hapa. (Picha na Ahmed Mahmoud).
Na Ahmed Mahmoud, Arusha
BARAZA la
madiwani wa halashauri ya jiji la Arusha,limemuagiza mganga mkuu wa jiji hilo
kuendesha kampeni maalumu ya chanjo ya ugonjwa wa Ini ,ambao ni hatari na hauna
dawa pia umekuwa ni tishio kwa maisha ya binadamu.
Agizo hilo
limetolewa na Mstahiki wa jiji la Arusha ,Kalisti Lazaro, Augosti 9 kwenye
kikao cha baraza hilo kilichofanyika kwenye ukumbi wa shule ya sekondari ya
Arusha na kusisitiza kwamba kampeni hiyo
ianze mara moja .
Ameiagiza
ofisi ya mganga mkuu wa Jiji hilo kuhakikisha wananchi wanashirikishwa
kikamilifu kupima afya zao na hataki kusikia mtu anapoteza maisha kutokana na
kutokuelimishwa ili wapime homa ya Ini
Mbunge viti
maalumu, Joyce Mukya,Alisema ugonjwa huo ni hatari kuliko Ukimwi hivyo Idara ya
afya isifanye mchezo na ugonjwa huo kwani unaua zaidi kuliko Ukimwi .
Madiwani
walisema kuwa wananchi hawana elimu juu ya ugonjwa huo ambao mpaka sasa haujawa na tiba bali tiba
yake ni chanjo hivyo wananchi wakipewa elimu watachukua tahadhari na kwenda
kupima afya zao kwenye vituo vya afya vya jiji la Arusha.
Akitoa
ufafanuzi Kaimu Mganga Mkuu wa Jiji la Arusha Dakta, Baraka Muondhe, alisema kuwa
Chanjo iliyokuwepo awali ilikuwa ikitolewa bure kata ya Daraja mbili ,lakini
sasa chanjo hiyo imekwisha na inatolewa na Zahanati binafsi .
Alisema kuwa
wameshapeleka maombi ya kupatiwa Chanjo hiyo kutoka MSD na itakapopatikana
itotolewa ambapo wananchi watachangia shilingi 15,000 na chanjo hiyo itatolewa
kwenye vituo vyote vya afya na Zahanati za jiji la Arusha.
Mstahiki
Meya wa Jiji la Arusha, Karisti Lazaro, ameitaka halmashauri ya jiji hilo
kuwakamata na kuwatia pingu watumishi wote watakaoonekana wanahujumu mapato ya
halmashauri hiyo kwa kuwa ni mafisadi wanaokwamisha maendeleo ya jiji hilo.
Ametoa agizo hilo kwenye kikao cha robo ya
mwisho yam waka 2018/19 cha baraza la madiwani alipokuwa akimpongeza mkurugenzi
wa jiji hilo ,Dakta Maulid Madeni ,kwa kusimamia ukusanyaji wa mapato na hatua
anazozichuku za kuwakamata watumishi wote wa halmashauri hiyo wanaojihusisha
na uhujumu wa mapato .
Meya
Karisti, amesema baraza hilo la madiwani linamuunga mkono kwa hatua hizo
anazozichukua za kuwabana watumishi wasio waadilifu ambao ni mafisadi
nakuongeza kwamba hata kama kuna madiwani
ambao waashirikiana na watumishi wasio waadilifu nao wachukuliwe hatua.
Amesema kuwa
mkurugenzi ameziba mianya lakini atambue kuwa
hivyo ni vita kubwa lakini baraza hilo linamuunga mkono kwenye vita
dhidi ya maafisa wote wanaohujumu halmashauri wapigwe pingu.
Ameipongeza
halmashauri hiyo kwa kukusanya mapato
kwa asilimia 105%ambapo halmashauri hiyo imekusanya shilingi bilioni
16.4 katika kipindi cha robo ya mwisho ya mwaka na hiyo inatokana na
ubunifu wa kuziba mianya ya upotevu wa
fedha.
Kwa upande
wake Mkurugenzi wa jiji ,Dakta Maulid Madeni,amesema halmashauri hiyo
imechangia shilingi milioni 140 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa bara bara
unaofanywa naTarura lengo ni kuzifanya bara bara zote za jiji ziwe za lami.
Amesema kuwa
halmashauri haiwezi kujiondoa kwenye
maswala ya utengenezaji wa bara bara ndio maana imetoa kiasi hicho cha
fedha kwa ajili ya kujenga bara bara hizo na kusisitiza kuwa Tarura, licha ya
kuondolewa halmashauri lakini bado inawajibika kwa halmashauri hiyo.
Madiwani
wakichangia wamesema kuwa Tarura, sasa tangia waondolewe halmashauri wamekuwa
huru sana na hawatoi usirikiano kwa madiwani na wana urasimu na hila za ajabu
ajabu .
Wamelalamikia
Tarura kumrundikia kazi mkandarasi mmoja na hivyo kushindwa kutengeneza na
kukamilisha barabara kwa viwango vya changarawe na moramu ziweze kupitika kwa
mwaka mzima na kutaka miradi ya barabara ifike mwisho
No comments:
Post a Comment