NA CLEZENCIA TRYPHONE
UONGOZI wa klabu hiyo a Yanga umekiri kuwakosa nyota wake watatu kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Towship Rollers.
Yanga inatarajia kuanza kutupa karata yake ya kwanza kesho katika Dimba la Taifa Dar es Salaam kuwakabili wababe hao kutoka Botswana katika mchezo huo wa kwanza.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam leo, Kaim Katibu Mkuu wa Yanga, Dismas Ten alisema, katika mchezo huo watawakosa nyota hao watatu kutokana na kutokuwa na leseni ya kuwawezesha kucheza mchezo huo.
Aliwataja nyota hao kuwa ni mlinda mlango Farouk Shikalo, Mshambuliaji David Molinga pamoja na beki Mustapha Seleman.
Aliongeza kuwa mpaka sasa mawasiliano yao na TFF ni mazuri hivyo muda wowote watapata leseni.
Aliongeza kwa kuwataka Wanayanga kujitokeza kwa wingi kuisapoti timu yao ili iweze kufanya vyema katika uwanja wa nyumbani.
No comments:
Post a Comment