Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndugulile, akiangalia bidhaa zinazotengenzwa na wanawake wa wilaya ya Kigamboni wakati wa uzinduzi wa Kamati ya Ulinzi ya Wanawake na Watoto ya Wilaya ya Kigamboni. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW).
Na Mwandishi Wetu, WAMJW
Naibu
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile amewaagiza watendaji wa Wilaya ya Kigamboni
kuhakikisha Kamati za ulinzi wa Wanawake na watoto zinatekeleza majukumu
yake ipasavyo kwa kuisadia
jamii ya wanakigamboni kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia .
Dkt. Ndugulile amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa
akizindua Kamati ya ulinzi ya wanawake na Watoto ya Wilaya ya Kigamboni pamoja
na Kampeni mpya ya Kitaifa ya kupinga vitendo vya ukatili dhidi ya
wanawake na watoto ijulikanayo kama Twende Pamoja inayolenga
kushirikisha wanaume na wanawake kwa lengo la kutoa elimu kwa jamii kupitia
mbinu anwai.
Aidha Dkt. Ndugulile amesisitiza kuwa Kamati hizo ikisimamiwa
vizuri itakuwa nuzo bora katika mapambano dhidi ya vitendo vya kikatili
vinavyozidi kushamiri kila siku nchini katika jamii na familia zetu.
Ameongeza kuwa kuwepo kwa elimu bure nchini kwa kiasi kikubwa
kumepunguza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake ikiwemo mimba na ndoa za
utotoni pamoja na uwepo wa Sheria inayotoa adhabu ya kifungo cha miaka 30 jela
kwa anayebainika kufanya vitendo hivyo.
''Ni matarajio yangu kwamba kampeni hii ya Kupinga Ukatilili wa
Kijinsia Kitaifa italeta mabadiliko makubwa kupitia jumbe mbalimbali
zilizoandaliwa kupitia muziki, machapisho, nyimbo, shuhuda na Semina
zitakazokuwa zinaendelea kutolewa kwenye majukwaa mbalimbali kipindi cha
kampeni’’ alisema Dkt. Ndugulile.
Dkt. Ndugulile pia ameagiza kutafutwa kwa wale waonafanya
vitendo vya kikatili katika wilaya ya Kigamboni na Tanzania kwa ujumla na
vyombo husika kusimamia na kuhakikisha wanawake na watoto wanapata haki zao.
Akizungumzia hali ya ukatili wa kijinsia nchini Dkt. Ndugulile
amesema taarifa ya hali ya Uhalifu nchini ya Mwaka 2017 inaonesha
kuwa jumla ya watu 41,416 waliofanyiwa ukatili wa kijinsia walitoa taarifa
kwenye vituo vya polisi ikilinganishwa na watu 31,996 waliofanya
hivyo mwaka 2016.
Dkt. Ndugulile ameyataja baadhi ya matukio ya ukatili
yaliyotolewa taarifa kuwa ni ubakaji, vipigo, matusi, ulawiti, kutupa watoto,
ukeketaji na kuwapa mimba wanafunzi na kuongeza kuwa kati ya
mataukio hayo 41,416 yaliyotolewa taarifa mwaka 2017 matukio 27,703
sawa na asilimia 67 yalifanywa dhidi ya wanawake na watoto.
Dkt. Ndugulile ameongeza kuwa asilimia 40 ya wanawake
wa umri kati ya miaka 15-49 wamefanyiwa ukatili wa kimwili au kingono mara moja
au zaidi katika kipindi hicho cha maisha wakati wanawake asilimia 20 wenye umri
miaka 15-49 wamefanyiwa ukatili wa kimwili katika kipindi cha miezi 12
iliyopita.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Sarah Msafiri
amesema kuwa Serikali ya Wilaya itahakikisha wanapambana na vitendo vya kikatili na amewaomba wanawake
kutoa taarifa ya vitendo hivyo na kuwataka kutofumbia macho vitendo hivyo na
kuacha vipite kwa mwavuli wa ndoa.
“Sisi Serikali tunaheshimu ndoa na dini zote ila tunaangalia
uhai wa mwananchi hivyo wanawake wenzangu nawaomba ndoa zisiwe sababu ya
kuendelea kufanyiwa vitendo vya kikatili na kuachana inawezekana” alisema Mhe. Sarah
Naye mmoja wa wnawake aliyefanyiwa vitendo vya kikatili Bi. Lucy
Sanga ameishukuru Serikali ya Wilaya ya Kigamboni kwa kumsaidia kupambana na
vitendo vya manyanyaso ambavyo anafanyiwa na mume wake.
“Mume wangu amekuwa akininyanyasa sasa kwa muda mrefu na
imefikia hatua ya kuficha vyombo vya kupikia na kunihamisha chumba chetu cha
kukaka na kumleta mama yake mzazi kutoka Musoma na yeye analala humo na me
nalala kwenye chumba cha watoto” alilalama Bi. Lucy
No comments:
Post a Comment