*Huzuni, simanzi, majonzi na vilio vyatawala mjini Morogorogo
HUZUNI, simanzi, majonzi na vilio vimetawala mjini Morogoro leo wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwaakiongoza
umati wa wananchi wa Manispaa ya Morogoro, mkoani Morogoro katika
mazishi ya wananchi waliofariki dunia kutokana na ajali ya moto wakati
wakichota mafuta yaliyokuwa yakimwagika baada ya lori la mafuta
kupinduka na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 71 huku wengine 59
wakijeruhiwa.
Mazishi
hayo yameanza kufanyika leo (Jumapili, Agosti 11, 2019) katika eneo la
makaburi la Kola Hill mjini Morogoro ambapo Waziri Mkuu amemwakilisha
Rais, Dkt. John Magufuli. Ametoa pole kwa wafiwa wote na amewaomba
wananchi wawe watulivu katika kipindi hiki cha maombolezo.
Akizungumza na wananchi katika ibada ya kuwaombea marehemu waliofariki katika ajali hiyo iliyotokea katika eneo la Msamvu mjini Morogoro iliyofanyika kwenye
viwanja vya hospitali ya mkoa wa Morogoro, Waziri Mkuu ametumia fursa
hiyo kuwashukuru viongozi na wadau mbalimbali kwa ushirikiano
waliouonesha wakati huu wa amajonzi.
Kufuatia
ajali hiyo iliyotokea jana saa 2 asubuhi baada ya lori lenye shehena ya
mafuta ya petrol kupinduka jirani na Kituo Kikuu cha Mabasi cha Msamvu
mjini Morogoro wakati dereva alipokuwa akijaribu kumkwepa mwendesha
pikipiki. Rais Dkt, Magufuli ametangaza siku tatu za maombolezo ya
Kitaifa kuanzia jana Jumamosi Agosti 10,2019 na bendera zote
zipeperushwe nusu mlingoti.
Mazishi
hayo yamehudhuriwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge,
Vijana, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, Waziri wa Nchi
OR-TAMISEMI, Selemani Jafo, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,
Isac Kamwelwe, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.
Wengine
ni Naibu Waziri wa Kilimo, Omary Mgumba, Naibu Waziri wa Nishati,
Subira Mgalu, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji
pamoja na wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, wabunge, viongozi wa dini na
wananchi wa mkoa wa Morogoro.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole , Shukuru Fabian ambye
ni mmoja wa majeruhi wa ajali ya moto wa lori la mafuta lililopinduka
katika eneo la Msamvu mjini Morogoro. Aliwajulia hali majeruhi wa ajali
hiyo kwenye hospitali ya mkoa wa Morogoro, Agosti 11, 2019. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa akimjulia hali, Hans Kifah ambaye ni mmoja wa majeruhi wa ajali
ya moto wa lori la mafuta lililopinduka kwenye eneo la Msamvu mjini
Morogoro. Aliwajulia hali majeruhi wa ajali hiyo kwenye hospitali ya
mkoa wa Morogoro, Agosti 11, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika ibada ya kuwaombea marehemu waliofariki katika ajali ya moto wa lori la mafuta lililoanguka katika eneo la Msamvu mjini Morogoro. Ibada hiyo ilifanyika kwenye viwanja vya hospitali ya mkoa wa Morogoro, Agosti 11, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika ibada ya kuwaombea marehemu waliofariki katika ajali ya moto wa lori la mafuta lililoanguka katika eneo la Msamvu mjini Morogoro. Ibada hiyo ilifanyika kwenye viwanja vya hospitali ya mkoa wa Morogoro, Agosti 11, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
No comments:
Post a Comment