Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia
Suluhu Hassan amesema kuwa Tanzania inajivunia kufanya kazi kwa karibu na Nchi
ya Rwanda kutokana na ukarimu mkubwa uliojengeka kwa muda sasa kwa Wananchi wa Nchi mbili hizo.
Makamu wa Rais amesema hayo leo alipokutana na Balozi wa Rwanda
Nchini Tanzania Mhe.Eugene Kayihura wakati Balozi Kayihura alipofika Ofisini
kwa Makamu wa Rais Ikulu Jijini Dar es salaam leo kwa ajili ya kumuaga Makamu
wa Rais Baada ya kumaliza muda wake wa kazi hapa Nchini.
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan amemuhakikishia
Balozi Kayihura kwamba Tanzania itaendelea kudumisha Uhusiano wa Nchi mbili
hizi uliodumu kwa muda mrefu sasa katika Nyanja mbalimbali za kimaendeleo na
kijamii hasa katika kuangalia fursa za kiuchumi pamoja na kuwa na uhusiano mzuri
wa huduma ya Fedha kati ya Rwanda na Tanzania.
Mhe. Samia amesema muda umefika sasa kushirikiana pamoja kwa
ajili ya kujenga Uchumi wa Mataifa haya, ambapo pia amempongeza Balozi Eugene
Kayihura kwa Ushirikiano Mkubwa alioutoa kwa Serikali ya Tanzania katika
kipindi chake chote cha kazi hapa Nchini na kumtakia kila la Heri kokote aendako
katika kituo chake kipya cha kazi.
Nae Nalozi Eugene Kayihura amemuhakikishia Makamu wa Rais
kwamba, Rwanda itaendelea kukuza na kudumisha Ushirikiano na Tanzania katika
pande zote za kimaendeleo na kuitakia Serikali ya Tanzania maandalizi mema ya
mkutano wa SADC.
IMETOLEWA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS.
No comments:
Post a Comment