HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 13, 2019

MILIONI MIA MBILI ZATUMIKA KULETA MAENDELEO KATA YA KIHESA

Diwani wa kata ya Kihesa manispaa ya Iringa Jully Sawani akiongea na mwandishi wa habari wa blog hii ofisini kwake Kihesa.

NA FREDY MGUNDA, IRINGA

Zaidi ya milioni mia mbili zimetumika kuleta maendeleo katika sekta ya elimu,miundombinu,afya na utamaduni katika kata ya Mapanda iliyopo katika jimbo la Mufindi kaskazini ikiwa ni kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi ya mwaka 2015 hadi 2020.

Akizungumza na blog hii diwani wa kata hiyo, Jully Sawani, alisemakuwa katika sekta ya elimu wamefanikiwa kujenga majengo mapya katika shule mbalimbali zilizopo katika kata hiyo kwaushirkiano wa serikali,wananchi na wadau mablimbali wa maendeleo waliopo katika kata hiyo.

“Nguvu ya wananchi ilikuwa ni mchanga na mawe tu,mfano shule ya sekondari ya kihesa ilikuwa inakabiliwa na ukosefu wa majengo,viti,meza za walimu na miundombinu ya shule haikuwa rafiki kabisa katika namna ya kutoa elimu bora kwa wanafunzi wa shule na hivyo hivyo katika shule za msingi ngome na Kihesa ambazo nazo zilikuwa zinakabiliwa na tatizo la vyoo na uchakavu wa miundombinu lakini tumefanikiwa kutatua tatizo hilo” alisema Sawani

Sawani alisema kuwa katika sekta ya afya amefanikisha zoezi la wazee na kupewa huduma bure,tatizo la madawa nalo wamefanikiwa kulitatua na kufanikiwa kuboresha huduma bora kwa kutoa elimu kwa wafanyakazi kutoa huduma bora kwa wagonjwa na wateja wote ambao wamekuwa wanapata huduma katika kituo hicho.

“Saizi ukienda katika kituo cha afya cha ngome unahudumiwa vizuri tofauti na ilivyokuwa hapo awali hiyo kutokana na elimu ambayo walipata wahudumu wote wa kituo hicho kutoka kwa wataalamu wa huduma makazini na ndio sababu ya sasa kutolewa huduma bora kabisa” alisema Sawani

Aidha Sawani alisema kuwa swala la barabara limekuwa changamoto kubwa kutokana na barabara hizo kuharibika mara kwa mara na zinatumia gharama kubwa kukarabati miundombinu hiyo lakini kuna barabra ya kutoka ngome kwenye shule sekondari ya Kihesa,mwachang’a kwenda  kanisani na majengo mapya.

“Ili kurahisisha maendeleo lazima kuwe na miundombinu bora hivyo nimepigana navyoweza kwa ushirikiano mkubwa na chama cha mapinduzi tumefanikiwa  kutatua kero hiyo kwa kiasi chake” alisema Sawani

Sawani alisema kuwa tatizo la maji linaelekea kutatuliwa kutokana najuhudi zinazofanywa kuhakikisha wananchi wa kata hiyo wanapata maji kwa kutumia mamilioni ya fedha kutoka kwa wadau na serekali ambapo wananchi wameshachanga na serikali tayari imeleta wataalamu kwa ajili ya kutatua kero hiyo.

No comments:

Post a Comment

Pages