Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa,
Meja Jenerali Martini Shiminzi Busungu kikombe cha ushindi wa jumla wa
Maonesho ya Wakulima Nane Nane yaliyohitimishwa na Waziri Mkuu kwenye
uwanja wa Nyakabindi mkoani Simiyu, Agosti 8, 2019. Kushoto ni Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka.wa tatu kushoto ni Waziri wa Kilimo,
Japhet Hasunga na wa nne kushoto ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga
Mpina.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI
MKUU, Kassim Majaliwa ameagiza kwamba kuanzia mwakani malipo yote ya
wakulima wa pamba yawe yanapitia benki ambapo wakulima wataingiziwa
fedha kupitia akaunti zao.
Hivyo,
ametumia fursa hiyo kuwasihi wakulima wafungue akaunti katika benki
mbalimbali zilizopo kwenye maeneo yao ili waweze kufanikisha mkakati
huo na pia kuhifadhi fedha zao kwa ajili ya matumizi ya baadae.
Waziri
Mkuu alitoa agizo hilo jana jioni (Alhamisi, Agosti 8, 2019) wakati
akizungumza na wananchi wa kijiji cha Luguru, wilayani Itilima mara
baada ya kukagua ghala la pamba la Chama cha Ushirika cha Msingi
cha Maendeleo.
Alitembelea
kijiji hicho kwa lengo la kujionea mwenendo wa uuzaji wa zao la pamba
katika Chama cha Msingi Maendeleo na alihakikishiwa kwamba kwa sasa
uuzaji wa pamba unaendelea vizuri
Waziri
Mkuu alisema ni vizuri malipo ya wakulima yapitie benki ili kuwawezesha
kupanga matumizi mazuri ya fedha zao na pia watapa fursa ya elimu ya
matumizi mazuri ya fedha.
Katika hatua nyingine,
Waziri Mkuu alieleza miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali
katika wilaya hiyo ukiwemo mradi wa ujenzi wa hospitali ya wilaya ambao
umefikia asilimia 95.
“Jumla
shilingi bilioni 1.5 zimetolewa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa
hospitali ya wilaya inayojengwa eneo la Nguno, ambapo majengo yote saba
ya kiupaumbele yamekamilika.”
Alisema
mwaka 2017/2018 Serikali ilitoa sh. bilioni 2.34 kwa ajili ya miradi ya
maji ya vijiji vya Lagangabilili, Mwamapalala, Kabale, Ikungulipu na
Isengwa, yote imekamilika na inatoa maji.
Alisema
mwaka 2019/2020 Halmashauri hiyo kupitia RUWASA imetengewa sh. bilioni
4.84 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya maji. Mradi huo
utavinufaisha vijiji 78.
Awali,Katibu
Mkuu wa Chama cha Msingi cha Maendeleo Luguru na Itubilo, Buzo Hussein
alimshukuru Waziri Mkuu kwani wakati wote amekuwa mstari wa mbele katika
kufuatilia kero mbalimbali zinazowakabili wakulima nchini na
kuzitafutia ufumbuzi.
“Hii
yote inatokana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na
Rais Dkt. John Magufuli inayowataka viongozi kufuatilia changamoto za
wananchi kwa vitendo na kuzitatua.”
Alisema
katika ghala la chama chao kuna jumla ya kilo 175,235 za pamba ambazo
zimekusanywa kutoka kwa wakulima ikiwa inasubiri wanunuzi.
No comments:
Post a Comment