HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 09, 2019

Mkwawa Trail Run watoa msaada Frelimo Hospital

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mlandege wakichukua maziwa baada ya timu ya waandaaji wa mbio za Mkwawa Trail Run 2019 walipotembelea shuleni hapo na kutoa zawadi mbalimbali.
Mratibu wa mbio za Mkwawa Trail Run, Amani Sapi Mkwawa, akigawa maziwa kwa akina mama katika wodi ya Mama na Mtoto hospitali ya Frelimo mjini Iringa, wakati waandaaji wa mbio hizo walipotembelea hospitalini hapo.
 

NA MWANDISHI WETU, IRINGA

TIMU ya Waandaaji wa Mbio za Mkwawa Trail Run 2019 imetembelea hospitali ya Flerimo mjini Iringa kuwajulia hali wagonjwa sambamba na kutoa msaada wa maziwa.

Mbio hizo za Mkwawa Trail Run zilifanyika kwa mara ya kwanza Agosti 4 mwaka huu Kalenga mkoani Iringa, zikiwa na malengo mbalimbali ikiwamo kuimarisha afya ya jamii na kutangaza utalii wa asili.

Akizungumza mjini hapa, Mratibu wa mbio hizo, Amani Sapi Mkwawa, alisema mbali na kutembelea Hospitali ya Flerimo wodi ya Mama na Mtoto, pia walitembelea shule ya Msingi Mlandege.

“Katika kuadhimisha Wiki ya Unyonyeshaji Maziwa, timu Mkwawa Trail Run kwa kushirikiana na Naibu Meya Meya Manispaa ya Iringa, tulitembelea wodi ya Mama na Mtoto Hospitali ya Frelimo na Shule ya Msingi Mlandege na kugawa maziwa na zawadi mbalimbali,” alisema Mkwawa na kuongeza.

Hii ni moja ya malengo ya Mbio za Mkwawa, kuboresha afya ya mtoto na jamii kwa ujumla.
Mkwawa, alibainisha kuwa Iringa ni miongoni mwa mikoa mitano inayoongoza kwa udumavu nchini.

Aliwashukuru wadau mbalimbali waliofanikisha mbio hizo ikiwamo Wakala wa Misitu (TFS), Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Asas Dairies Ltd, Aga Khan Hospital, Tanapa, Selcom na wengineo.

Mbio hizo ambazo zimefanyika kwa mara ya kwanza mwaka huu, zitakuwa zikifanyika kila mwaka mkoani Iringa.

No comments:

Post a Comment

Pages