MWANAMKUU
MBAROUK, TANGA
MABINGWA watetezi wa mashindano ya Voa Marmar Best Cup,
Mtonga FC wamelazimishwa sare ya bao 1-1 na Bodaboda FC katika mchezo wa kwanza
wa hatua ya robo fainali uliyochezwa
uwanja wa Matondolo Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga.
Mchezo huo uliokuwa wa kuvutia kutokana na wachezaji wa timu
hizo kuonyesha ufundi wa kutandaza soka hasa la chini chini, jambo ambalo liliwafanya
mashabiki kupata burudani safi.
Bodaboda FC ilianza kupata bao mapema dakika ya tano lililofungwa
na straika wake, Makange Aloice kabla ya mabingwa watetezi kusawazisha dakika
ya 26 kupitia Semi Gasper.
Mkurugenzi wa mashindano hayo, Martin Mhina, alisema kadiri
michuano hiyo inavyoendelea ndivyo ushindani unavyoongezeka na kuwaomba
mashabiki kuzidi kujitokeza kushuhudia vipaji.
No comments:
Post a Comment