NA
MWANAMKUU MBAROUK, TANGA
KOCHA wa Sahare All Stars, Abdallah Kessy ‘Villas Boas’
amesema hatishwi na majina ya timu walizopangwa nazo kundi moja Ligi Daraja la
Kwanza (FDL), kwa sababu wamejipanga.
Sahare All Stars ambayo ni msimu wake wa kwanza kucheza FDL
na ipo Kundi B ikiwa na Arusha FC, Geita Gold FC , Gipco FC, Green Warriors,
Gwambina FC, Mashujaa FC, Mawenzi FC, Pamba FC, Rhino Rangers, Stand United FC
na Transit Camp FC.
Villas Boas, alisema malengo yao msimu huu ni kupanda Ligi
Kuu (TPL), na si vingine, kwa hiyo wamejiandaa kupambana na timu zozote
watakazokutana nazo kwa sababu uwezo wa kufanya hivyo wanao.
Alisema, kwa sasa anawaanda wachezaji wake kwa mapambano tu
na si vingine na kwa uzoefu wake anafahamu FDL hakuna mchezo mwepesi wala timu
rahisi, la muhimu ni kujiandaa kwa mapambano tu .
“Michezo yetu yote iwe nyumbani au ugenini tutacheza kama
fainali, lengo likiwa ni kupata matokeo mazuri na kupanda Ligi Kuu, kwa hiyo
tunaomba mashabiki na wadau wa soka kutuunga mkono hatua kwa hatua,” alisema
Villas Boas.
Kocha huyo, alisema hata usajili wa wachezaji waliowaongeza katika
dirisha kubwa, ulizingatia vigezo hivyo kwa hiyo wamekamilika kila idara na
wapo tayari kupambana na timu yoyote katika kundi lao.
No comments:
Post a Comment