NA MWANDISHI WETU
UONGOZI wa Namungo FC inayoshiriki Ligi Kuu
Tanzania Bara (TPL), kwa mara ya kwanza, unatarajia kutambulisha kikosi chao
cha msimu ujao kwa kucheza na Polisi Tanzania Agosti 10, kwenye Uwanja wa
Majaliwa, wilayani Ruangwa mkoani Lindi.
Namungo FC yenye maskani yake wilayani Ruangwa
mkoani Lindi, ni miongoni mwa timu ambazo zinapewa kipa umbele cha kufanya
msimu ujao kutokana na usajili waliofanya na kiwango walichokionyesha msimu
uliopita Ligi Daraja la Kwanza (FDL).
Siku hiyo ambayo mashabiki wa Namungo wataingia
bure uwanjani hapo, itaambatana na mchezo ya kujipima nguvu, dhidi ya Polisi
Tanzania ambao wamepanda daraja msimu huu kutoka Kundi B la FDL.
Akizungumza na
TanzaniaDaima, Mwenyekiti wa Namungo FC, Hassani Zidadu, alisema alisema
wameamua kutambulisha kikosi chao siku hiyo ili wakazi wa Ruangwa wawatambue
nyota wao kabla ya kuanza kwa ligi msimu ujao.
“Tunatarajia kutambulisha kikosi chetu chote na
Benchi la Ufundi tulikuwa bado hatujamaliza taratibu za usajili, hivyo
tutafanya utambulisho ili kuwajuza mashabiki kukifahamu kikosi chetu.
“Kikubwa ni wakazi wa Ruangwa kujitokeza kwa wingi
siku hiyo kuona timu yao na kiingilio ni miguu yako tu! Maana tunatakiwa
tujitokeze kwa wingi,” alisema.
No comments:
Post a Comment