NA Mwandishi Wetu, Mtwara
OMBI
la mirathi kati ya Mohamed Mussa dhidi ya Jamaldin Mtonya na Kuruthum
Mtonya lilililokuwa lisikilizwe Juni 11, Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara
sasa linasikilizwa kesho.
Ombi
hilo liliahirishwa kusikilizwa Juni 11 kwa sababu Jaji anayesimamia
shauri hilo, Wilfred Dyansobera kwenda mkoani Kagera kikazi.
Kwa
mujibu wa taarifa kutoka Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara shauri hilo
litasaikilizwa na mahakama hiyo kama ilivyopangwa ambako awali lilikuwa
lianze kusikilizwa Mei 9 halikuskilizwa kwa Sababu ya kukosekana kwa
mpingaji wa ombi la usimamizi wa mirathi hiyo, Jamaldin Mtonya aliyekuwa
akiumwa Malaria na kutuma mwakilishi ambaye ni Hassan Salum Namkami
aliyewakilisha taarifa za kuumwa kwake.
Katika
shauri hilo Jaji Dyansobera baada ya kupokea taarifa hiyo, alimuuliza
mwakilishi kwamba umekuja na cheti kinachoelezea kuumwa kwa Jamaldin,
akaeleza mahakamani hapo kwamba hakuja nacho.
Baada
ya kujibiwa hivyo, Jaji Dyansobera alimuuliza Mohamed Mussa wachukue
hatua gani baada ya kukosekana kwa mpingaji, akajibu anaiachia mahakama
iamue.
Swali
kama hilo akaulizwa pia Kuruthum naye akajibu kwamba mahakama ndio
yenye uamuzi kuhusu mwenendo wa kesi hiyo ndipo jaji akaeleza kwamba
shauri hilo litasilikizwa Juni 11 mwaka huu.
Kabla
ya Mei 9 mlalamikaji Mohamed Mussa aliwasilisha rufaa mahakamani hapo
baada ya Mahakama ya Wilaya Tandahimba kutomtendea haki aliyoitaka
ikiwemo kutoa hukumu iliyotolewa Oktoba 27, 2018 ambayo ilikuwa siku ya
Jumamosi siku ambayo si ya kazi.
Baada
ya Mohamed Mussa kuwasilisha maombi ya kuwa msimamizi wa mirathi hiyo,
Jaji Dyansobera aliwataka walalamikiwa kuwasilisha mapendekezo yao
kuhusu usimamizi wa mirathi hiyo jambo ambalo walilitekeleza.
Rufaa
hiyo yenye namba 23/2018 inahusu usimamizi wa mirathi ya marehemu Mussa
Mtonya ambaye alikuwa na mashamba makubwa likiwemo la ukubwa wa ekari
118, ekari 80 na mali nyinginezo.
Awali
mvutano wa pande hizo mbili umetokana na mlalamikaji, Mohamed Mussa
kuomba kuwa msimamizi wa mirathi ya marehemu baba yao aliyefariki dunia
mwaka 2002 ambaye aliacha watoto 20.
Katika
hoja zake mahakamani hapo, Jamaldin anapinga kaka yake Mohamed kuwa
msimamizi wa mirathi hiyo na kuhitaji dada yake Kuruthumu Mussa ndiye
awe msimamizi wakati hajawasilisha maombi ya kutaka kufanikisha hatua
hiyo.
Katika
Rufaa yake hiyo Mahakama Kuu, Mohamed Mussa anaeleza kwamba kwa kuwa
yeye ameomba kusimamia mirathi ya marehemu baba yake, ndio maana
aliwasilisha maombi hayo tangu mahakama ya mwanzo iliyoko wilayani
Tandahimba mkoani Mtwara lakini dada yake hakuomba lakini anashangaa
wanamlazimisha.
Kwa
upande wake Kuruthum amewasilisha ombi la kukataa kuwa msimamizi wa
mirathi hiyo kwa sababu hakuhitaji kutekeleza hatua hiyo ambayo
inawezekana ikatekelezwa na kaka yake.
No comments:
Post a Comment