NA SULEIMAN MSUYA
MKURUGENZI
wa Sekretarieti ya Siasa, Ulinzi na Usalama wa Jumuiya ya Maendeleo
Kusini mwa Afrika (SADC), Jorge Cardoso amesema jumuiya hiyo
itashirikiana na nchi wanachama kukabiliana na biashara ya dawa za
kulevya .
Akizungumza na
waandishi wa habari leo Cardoso alisema wanatambua njia nyingi
zinazotumiwa na waingizaji wa dawa za kulevya katika ukanda wa SADC,
ikiwamo njia ya Pwani ya Kusini Mashariki mwa Afrika, ambazo wamekuwa
wakishirikiana na Serikali za nchi husika kudhibiti uingizaji wa dawa
hizo.
Alisema biashara ya
dawa za kulevya ni tatizo kubwa na linaathiri nguvu kazi katika nchi
wanachama ila wamekuwa wakifanya jitihada za makusudi kukabiliana na
tatizo hilo.
"Tumekuwa
tukishirikiana na jumuiya ya kimataifa kuhakikisha tunadhibiti njia zote
zinazotumika kuingiza dawa za kulevya katika nchi zetu,"alisema.
Mkurugenzi
huyo alisema zipo njia za kuingiza dawa kutoka Amerika ya Kusini, Ulaya
na kwingineko ila jambo la faraja ni kuwa wanapata taarifa kila
kukicha.
Cardoso alisema
wafanyabiashara wa dawa hizo wamekuwa wakibuni mbinu za kupata njia mpya
kila wanapodhibitiwa, lakini wamekuwa wakishirikiana na jumuiya
nyingine kukabiliana nao.
Aidha, alisema Polisi wa Kimataifa (Interpol) katika mkusimamia na kudhibiti bishara hiyo wamekuwa msaada mkubwa.
Alieleza kuwa wamekuwa pia wakishirikiana na vyombo vya Umoja wa Mataifa (UN) vinavyoshughulika na udhibiti wa dawa hizo.
Alisema
kuhsu suala la demokrasia katika nchi wanachama, sekretarieti hiyo
imeku ikisimamia na kuhakikisha viwango vinavyokubalika na nchi
wanachama vinalindwa, kw akufuatilia taratibu zote za maandalizi,
uchaguzi na baada ya uchaguzi kisha kutoa mapendekezo.
Alisema
sekretarieti yake imekuwa ikisimamia masuala yanayohusu ushirikiano
katika usalama pale yanapotokea majanga mbalimbali, kama ilivyotokea kwa
kimbunga Idai, kilichosababisha maafa kwa zaidi ya watu 300,000 nchini
Msumbiji, Malawi na Zimbabwe, ambao walihitaji misaada ya haraka.
Serikali
ya Tanzania ilikuwa mstari wa mbele katika kutoa misaada ya halki na
mali, ikiwamo misaada ya chakula na dawa kwa watu walioathiriwa na
kimbunga hicho.
No comments:
Post a Comment