Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) Filbert
Bayi (kushoto) akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari na wachezaji wa timu ya Taifa inayotarajia kushiriki mashindano
ya All African Games nchini Morocco (hawapo pichani) wakati wa kuiaga timu hiyo
mapema hii leo jijini Dar es Salaam, katikati ni Rais wa Kamati ya Olimpiki
nchini, Gulam Abdalla Rashid na kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo,
Yusuph Singo.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Yusuph Singo akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari na
wachezaji wa timu ya Taifa inayotarajia
kushiriki mashindano ya All African Games nchini Morocco wakati wa kuiaga timu
hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Yusuph Singo
(kushoto) akimkabidhi bendera ya Taifa nahodha wa timu ya Taifa inayotarajia
kushiriki mashindano ya All African Games nchini Morocco, Gabriel Geay wakati
wa hafla ya kuiaga timu hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Yusuph Singo
(kushoto) akimvalisha bendera ya Taifa
nahodha wa timu ya Taifa inayotarajia kushiriki mashindano ya All African Games
nchini Morocco, Gabriel Geay wakati wa hafla ya kuiaga timu hiyo mapema hii leo
jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wachezaji watakaoshiriki mashindano ya All
African Games nchini Morocco katika mchezo wa judo na riadha wakimsikiliza
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Yusuph Singo (hayupo pichani) wakati wa
hafla ya kuiaga timu hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam. (Picha na WHUSM – Dar es Salaam).
No comments:
Post a Comment