Mashabiki wa Simba wakishangilia timu yao wakati ikipambana na UD Songo kutoka Msumbiji katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF CL) uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Timu hizo zilitoka sare ya 1-1. Kwa matokeo Simba imetolewa katika mashindano hayo na UD Songo inasonga mbele kwa faida ya bao la ugenini. (Picha na Said Powa).
Mshambuliaji wa Simba, Clatous Chama, akimtoka mchezaji wa UD Songo katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF CL) uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Timu hizo zimetoka sare ya 1-1.
Shabiki wa Simba akiwa amebebwa na watu wa huduma ya kwanza wakati wa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Simba na UD Songo uliopigwa leo kwenye dimba la taifa jijini Dar es Salaam. Simba imeondolewa kwenye michuano hiyo kwa goli la ugenini.
Mshambiliaji
wa Simba, Meddie Kagere, akiwa amejiinamia mara baada ya kipyenga cha
kumalizika kwa mchezo kati ya timu hiyo na UD Songo ya Msumbiji
uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Simba
imeondolewa kwenye michuano hiyo kwa bao la ugenini baada ya kutoka sare
ya 1-1. (Picha na Said Powa).
Wachezaji
wa Simba wakimpokonya mpira mlinda mlango wa UD Songo, Leonel Pindula,
mara baada ya beki wa Simba Erasto Nyoni kuisawazishia timu yake kwa
mkwaju wa penalti katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Timu hizo zilifungana 1-1.
No comments:
Post a Comment