Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti, ametoa maagizo kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera kuwasaka na kuwamata watu wote waliohusika na zoezi la uchukuaji wa mafuta katika lori lililoanguka.
Wananchi wakiwa katika hekaheka za kuchota mafuta katika lori lililoanguka mkoani Kagera.
Picha tofauti zikionesha wananchi wakichota mafuto kutoka katika loiri lililoanguka mkoani Kagera.
Na Lydia Lugakila, Kagera
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti, amemuagiza Kamanda wa Polisi mkoani Kagera kufanya msako mkali wa kuwabaini wananchi katika eneo la Benako wilayani Ngara mkoani hapa waliohusika katika zoezi la kuchota mafuta au kujaribu kuchota mafuta kwenye lori la mafuta lililopata ajali Agosti 25.
Mkuu wa Mkoa Brigedia Jenerali Marco Gaguti, amesema kuwa ni hali ya kustajabisha na kuuzunisha kutokana na tukio hilo lililowahusisha wanawake, wanaume na watoto walioonekana katika clip ya video inayotembea kwenye mitandao mbali mbali ya kijamii ikionyesha baadhi ya wananchi katika eneo la Benako wilayani Ngara mkoani hapa wakichota mafuta kwenye lori la mafuta lililopata ajali August 25, 2019.
Mkuu huyo wa mkoa amesema kuwa wananachi walionekana katika clip ya video wakichota mafuta ni pamoja na wanawake, wanaume na watoto wakiwa na vidumu pamoja na ndoo.
Imeelezwa kuwa ajali hiyo imelihusisha gari aina fuso 456 CMI lililokuwa likinaendeshwa na dreva mwenye asili ya kiarabu na kuwa Dreva huyo amepelekwa katika hospitali iliyopo wilayani humo ili kupata matibabu.
Kufuatia hali hiyo Brigedia Marco Gaguti amemuagiza Kamanda wa Polisi mkoani hapa kufanya msako mkali katika maeneo ya vijiji jirani na kuhakikisha wahusika waliojaribu wa walochota mafuta wanatiwa nguvuni.
‘’Hali hii inadhihilisha kwamba kuna baadhi ya wananchi hawajajifunza au hawataki kujifunza kutokana na ajali iliyotokea August 10 mwaka huu huko mkoani Morogoro hivyo basi Naagiza Wahusika hao wakamatwe mara moja ili wafikishwe katika vyombo vya sheria.
Aidha mkuu wa mkoa ametumia fulsa hiyo kutoa onyo kwa wanakagera na watanzania wote kwa ujumla kutambua kuwa ni vyema kujiepusha na Matukio ambayo yanaweza kusababisha madhara makubwa katika taifa hili.
Amesema kuwa Mkoa wa Kagera unazo njia za kwenda nchi jirani za Rwanda ,Burundi, na Uganda na kumekuwa na magari mengi na makubwa ya bidhaa mbali mbali ikiwemo mafuta na Magari hayo hutumia njia hizo hivyo ni vyema kujiepusha na matukio yoyote yale ambayo kwa njia moja ama nyingine yanayoweza kuleta madhara na kuleta vilio katika taifa la Tanzania.

No comments:
Post a Comment