HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 24, 2019

TAEC yatoa mafunzo ya mionzi kwa taasisi

MKURUGENZI Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC), Prof. Lazaro Busagala (aliyekaa katikati), akifurahia jambo na washiriki wa mafunzo ya jinsi ya kujilinda na mionzi wakati wanapotumia mashine  za kuchunguzia mizigo. 
 
Mafunzo hayo ya siku tano yaliyohitimishwa jana, yamelenga kuongeza uelewa wa pamoja juu ya uthibiti wa mionzi katika mashine hizo yakihudhuriwa na wafanyakazi 9, wakiwamo nane kutokea Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na mfanyakazi mmoja (1) kutoka katika Hotel ya Arusha Four Point by Sheraton.

Zoezi la mafunzo haya, linatazamiwa kufanywa kwa mamlaka zote nchini zilizo na machine za namna hiyo kama viwanja vya ndege, mahotelini, Mamlaka ya Bandari Tanzania (THA) na sehemu za mipakani kama ilivyoinishwa kwenye Sheria Na. 7 ya mwaka 2003

No comments:

Post a Comment

Pages