Na Mwandishi Wetu, Mbeya
Serikali
kupitia Wizara ya Afya, Maybe ya Jamii, Jinsia, Wazee na Wat's
inaendelea na zoezi usajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kwa Kanda
ya Nyanda za Juu Kusini ili kuhakikisha kuwa asasi zote zinazofanya
shughuli za kijamii na kiuchumi katika ngazi za jamii zinajisajili chini
ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Namba 24 ya mwaka 2002 kama
ilivyofanyiwa mabadiliko ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali
Na. 3 ya mwaka 2019.
Hayo
yamesemwa leo jijini Mbeya na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
Serikalini Bw Erasto Ching'oro alipokuwa akizungumza na waandishi wa
habari kuhusu zoezi la usajili wa NGOs zilizo nje ya Sheria.
Bw.
Erasto Ching’oro amesema kuwa mapema leo kuwa Wizara iko katika hatua
ya mwisho ya kukamilisha usajili wa NGOs zilizosajiliwa awali chini ya
Sheria nyingine ambazo zinatakiwa kukamilisha usajili wao chini ya
Sheria ya NGOs kabla ya tarehe 31 Agosti, 2019.
Ameongeza
kuwa usajili katika Kanda ya Nyanda za juu kusini utafanyika kwa muda
wa siku tano kuanzia tarehe 13- 17 Agosti, 2019 na utajumuisha wadau wa
NGOs kutoka mikoa ya Rukwa, Ruvuma, Iringa, Njombe, Katavi, Songwe na
Mbeya pamoja na maeneo mengine na unafanyika Ukumbi wa Mikutano wa Mkapa
jijini Mbeya.
Bw.
Ching’oro ametoa wito kwa wadau wa mashirika yasiyo ya kiserikali
kutumia kikamilifu muda uliotolewa kusajili NGOs zao ili kukamilisha
zoezi la kuhamisha usajili katika muda elekezi wa miezi miwili ambao
ulianza tarehe 1 Julai, 2019 na utahitimishwa tarehe 31 Agosti, 2019.
"Mabadiliko
ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Namba 3 ya mwaka 2019
inayataka Mashirika yote yaliojisajili chini ya Sheria nyinginezo
kuhakikisha yanakamilisha uhamisho wao ndani ya kipindi cha miezi miwili
kuanzia siku ya tarehe 1 Julai, 2019 hadi 31 Agosti, 2019 ili kuendelea
kuwa na haki na hadhi ya kuendesha shughuli zao katika jamii kwa
kuzingatia Sheria, taratibu na kanuni za Mashirika Yasiyo ya
Kiserikali. Alisisitiza Bw.Ching’oro.
Ameongeza
kuwa zoezi la kuhuisha usajili wa mashirika yanayofanya kazi za kijamii
na kiuchumi katika ngazi ya jamii lina umuhimu ukubwa maana litawezesha
kuwa na matumizi bora ya rasilimali za nchi kwa kuwa na mgawanyo wenye
uwiano wa afua mbalimbali za huduma za kijamii, wananachi watahamaishwa
kuchangia maendeleo yao, kukuza ajira na kuongeza maarifa katika
uendeshaji wa miradi ya kijamii na kukuza uwazi na uwajibikaji kwenye
miradi shirikishi jamii.
Usajili
huu ulizinduliwa Kitaifa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb.) katika Kanda
ya Mashariki jijini Dar es salaam mapema tarehe 10 Julai, 2019 na
unahitimishwa katika Kanda ya Nyanda za Juu kusini mkoani Mbeya siku ya
tarehe 17 Agosti, 2019 jijini Mbeya.
No comments:
Post a Comment