HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 19, 2019

WANAFUNZI ELIMU YA JUU WAASWA

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, amewasa wanafunzi wanokwenda kusoma nchini China kuzingatia masomo. 
Waziri Ndalichako ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kuwaaga wanafunzi 61 waliopata ufadhili wa masomo nchini China. 
 
 'Naomba mtakapokwenda China mtumie nafasi hiyo vizuri kwani wapo vijana wengi wa kitanzania waliokosa nafasi hiyo. alisema Prof. Ndalichako.

Aidha Prof. Ndalichako alitoa ushauri kwa wanafunzi waliochaguliwa kwenda katika masomo ya elimu ya juu kwa kufanya bidii ya masomo ili kupata ujuzi, maarifa pindi watakaporudi kuja kushirikiana na serikali katika nyanja mbalimbali.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, akizungumza na baadhi ya wanafunzi walipota ufadhili wa masomo ya elimu ya juu nchini China, wakati wa hafla ya kuwaaga wanafunzi 61 iliyofanyika jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande).
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, akibadilishana mawazo na Balozi wa China, Wang Ke, wakati wa hafla ya kuwaaga wanafunzi waliopata ufadhili wa masoko ya elimu ya juu nchini China.
 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, akitoa hotuba yake wakati wa hafla ya kuwaaga wanafunzi waliopata ufadhili wa masoko ya elimu ya juu nchini China.
Balozi wa China, Wang Ke, akizungumza na baadhi ya wanafunzi walipota ufadhili wa masomo ya elimu ya juu nchini China, wakati wa hafla ya kuwaaga wanafunzi 61 iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako na Balozi wa China, Wang Ke (katikati) wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi waliopata ufadhili wa masomo ya elimu ya juu nchini China.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako na Balozi wa China, Wang Ke (katikati) wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi waliopata ufadhili wa masomo ya elimu ya juu nchini China.
  Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako na Balozi wa China, Wang Ke, wakifurahia jambo.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako (kulia), akimkabidhi Balozi wa China, Wang Ke, zawadi ya picha inayoonyesha mbuga ya wanyama pamoja na mlima Kilimanjaro.



 

No comments:

Post a Comment

Pages