Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),
Selemani Jafo, akikaribishwa na Meneja wa NMB Kanda ya Kati, Nsolo Mlozi.
Meneja
Mwandamizi wa Wateja Wadogo na wa Kati wa Benki ya NMB, Ally Ngingite,
akisalimia Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo, kabla ya kufungua Mkutano wa Walimu
Mkoa wa Dodoma uliofanyika jijini humo.
Meneja Mwandamizi wa Wateja Wadogo na wa Kati wa Benki ya NMB, Ally Ngingite, akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo, kufungua Mkutano wa Walimu Mkoa wa Dodoma uliofanyika jijini humo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo, akizungumza kwenye ufunguzi wa TEACHERS DAY Mkoa wa Dodoma iliyoandaliwa na Benki ya NMB.
Meneja Mwandamizi wa Wateja Wadogo na wa Kati wa Benki ya NMB, Ally Ngingite, akimkabidhi zawadi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo (kulia), mara baada ya kufungua Mkutano wa Walimu Mkoa wa Dodoma uliofanyika jijini humo.
Meneja Mwandamizi wa Wateja Wadogo na wa Kati wa Benki ya NMB, Ally Ngingite (kulia), akibadilishana mawazo na Meneja wa NMB Kanda ya Kati, Nsolo Mlozi (kushoto) na katikati ni Ofisa wa benki hiyo.
Baadhi ya Walimu Mkoa wa Dodoma wakishiriki Mkutano wa Teachers Day.
Dodoma, Tanzania
Serikali imeitaja
benki ya NMB kuwa miongoni mwa taasisi zilizofanikisha makusanyo ya fedha kwa
mwaka 2018/19 kwa kuwa benki hiyo haina tofauti na Wizara ya Tamisemi kwa
kufika maeneo yote nchini.
Kauli hiyo
ilitolewa jana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi) Seleman Jafo, wakati
akizungumza na walimu zaidi ya 300 kutoka halmashauri za wilaya mkoani Dodoma
katika siku ya mwalimu ambao walikutanishwa na benki ya NMB.
Waziri Jafo alisema
uamuzi wa benki hiyo kwenda nchi nzima na kufungua matawi, mawakala pamoja na
kuongeza ATM, ulisaidia kwa watu kuzifikia kwa urahisi huduma za kibenki pamoja
na halmashauri kuitumia kwa makusanyo yake.
Hivi
karibuni
Jafo alitangaza mapato ya serikali kutoka katika halmashauri yakipanda
kutoka
asilimia 73 ya mwaka 2017 hadi kufikia asilimia 81 mwaka 2018, juzi
kwenye za mapato katika mmalaka ya serikali za mitaa tumekusanya
takriban billioni 664 sawa na asilimia 91 kiasi ambacho hakijawahi
kufikiwa. Ninyi NMB mmetusaidia kwa hili," alisema Waziri Jafo.
Kuhusu benki
ya NMB alisema ni miongoni mwa taasisi zinazofanya vizuri hapa nchini ikiwa na
wateja zaidi ya 3.5 milioni pamoja na matawi 229 ambayo ni zaidi ya halmashauri
zilizopo ingawa aliwataka waongeze wateja na kuagiza kitengo cha utafiti kufanya
kazi yake vizuri.
Kuhusu mikopo
alisema kuna kilio kutoka kwa watumishi kuhusu riba kubwa ya mikopo kwenye mabenki
yote nchini kwani wanatoza kiwango ambacho si rafiki kwa wafanyakazi jambo
linalopekea malalamiko na wengine kujutia uamuzi wa kukopa.
“Naomba
suala la riba mliangalie, haiwezekani riba ya mfanyakazi ikawa sawa na
anayefanya biashara, ndiyo maana mnasababisha walimu kuingia madeni kwenye
visaccos vingine hadi wanaacha kadi zao huko mwisho wa siku wengine wanataka kujinyonga,
tafakarini ikibidi mfike hata kwenye single digit,” alisema Jafo.
Katika hatua
nyingine aliwataka walimu kutumia mishahara yao kwa utaratibu na kuacha maisha
ya kuiga kwani ndiyo yanayowapelekea kwenye madeni makubwa.
Meneja wa
NMB Kanda ya kati Solo Mlozi alisema benki hiyo imejipanga kuwafikia Watanzania
mahali walipo kwa kutumia mawakala wake na kuendelea kuboresha huduma zao kwa
kadri iwezekanavyo.
Mlozi alimwomba
Waziri kufikisha ujumbe wao serikalini ili waendelee kuiamini benki hiyo na
kufanya nayo kazi kwa kuwa serikali ina hisa ya asilimia 31 ndani yake hivyo na
mambo yaliyozungumzwa watashauriana ili kuwapunguzia mzigo Watanzania.
Awali Meneja
Mwandamizi wa wateja wadogo Ally Ngingite alisema benki hiyo imeweka utaratibu kuwafikia
walimu kama sehemu ya wateja na kusikiliza changamoto zao.
Ngingite alisema
mpango huo ulianzia Jijini Dar es Salaam,Pwani na jana Dodoma kabla ya kwenda
mikoa mingine ikiwemo Zanzibar huku akitaja benki kusogeza huduma zaidi kw
akutumia simu za mkononi.
No comments:
Post a Comment