HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 24, 2019

WABUNGE SHINYANGA WATAKIWA KUELEZA WALICHO KIIBUA KATIKA MAJIMBO YAO

Na  Gaudens Msuya, Kishapu

MAKAMU  wa pili wa Rais  Zanzibar  Balozi Self Ali Idd amewataka wabunge waeleze walivyotekeleza ilani  ya chama cha Mapinduzi kwa kuelezea nini walichokifanya  wao na kupitia fedha za mkufo wa jimbo sio kuelezea miradi inayotekelezwa na serikali.

Miradi inyotekelezwa na serikali itatangazwa na mkuu wa mkoa  Zainabu Telack kwenye kamati kuu ya  siasa ya mkoa  na wabunge waeleze miradi  au wamekisaidiaje  chama kwa kutumia fedha zao mfukoni au  mfuko wa jimbo.

Balozi  Idd  ambaye ni mlezi wa chama cha Mapinduzi  kwa mkoa wa Shinyanga na mjumbe wa kamati kuu taifa ya chama hicho  aliyasema hayo  juzi kwenye  kwenye mkutano wa hadhara  uliofanyika kwenye kijiji cha Somagedi wilayani Kishapu baada ya mbunge wa jimbo hilo Suleiman Nchambi  kueleza utekelezaji wake katika ilani.

Balozi  Idd aliwataka  wabunge waeleze walivyotekeleza ilani  ya chama cha Mapinduzi kwa kuelezea nini walichokifanya  wao na kupitia fedha za mkufo wa jimbo sio kuelezea miradi inayotekelezwa na serikali  ili wananchi wafahamu.

“Mimi nitakuwa mkali  ndani ya chama kwa mbunge ambaye hafanyi vizuri na yule mbunge ambaye anakuja  mpaka asikie kiongozi wa kitaifa anakuja  nae mbio  anakuja hao hatuta wavumilia  hata chama kilikwisha waonya tabia hizo waonekane  majimboni wasikimbie wapiga kura wao”alisema  Balozi Idd.

Alisema chama kilikwisha toa agizo kuwa wabunge wote wakae kwenye majimbo yao  nayeye  anaangalia utendaji  kazi  wa  mtu atakapo fika kwenye kikao cha kamati kuu katika kuwajadili wabunge atakapo ulizwa  kuhusu mkoa wa Shinyanga kama mlezi wake itabidi aseme ukweli kwa wasiofanya vizuri na wanaofanya vizuri katika utekelezaji wa ilani.

Aliwapongeza  baadhi ya wabunge akiwemo mbunge Azza Hilali  kuwa amefanya kazi nzuri kwa wananchi wa mkoa wa  Shinyanga  baada ya kueleza kutoa kiasi cha shilingi millioni 130  kwa jimbo la kishapu pekee huku akimueleza  ulichaguliwa kuwatumikia wananchi.

Mbunge wa jimbo la Kishapu Suleima Nchambi  alimkabidhi balozi  Idd  mifuko 1200 ya saruji na mabati 400 kwaajili ya kata zote 25 ili kuweza kukamilisha maboma  yaliyoanzishwa kwa nguvu za wananchi  huku akieleza kuwa tangu kuachakuliwa kwake uchaguzi mkuu mwaka 2015 ameweza kutoa mifuko 8000 ya saruji.

“Katika utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi nimeweza kutoa fedha zangu mfukoni na mfuko wa jimbo kiasi kisichopungua millioni 100 katika kukisaidia chama na  kutekeleza miradi ya maendeleo nakujumuika na wananchi wangu hata wao ni mashahidi”alisema mbunge Nchambi.

No comments:

Post a Comment

Pages