HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 17, 2019

Dk. Kijazi aeleza faida za hali ya hewa SADC


 
NA MWANDISHI WETU

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agnes Kijazi, amesema ushiriki wa mamlaka hiyo kwenye vikao vya Nchi jumuiya za Maendeleo

Dk. Kijazi alisema hayo mapema leo alipozungumzia kuanza kwa mkutano wa baadhi ya mawaziri wa nchi wanachama Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), ulioanza leo jijini Dar es Salaam.

"Tunaposhiriki taifa litaboresha  huduma za hali ya hewa kupitia mafunzo ya hali ya hewa yanayotolewa kwa nchi wanachama wa SADC kupitia programu mbalimbali za hali ya hewa.

"Tutapata miundombinu ya hali ya hewa inayotolewa kupitia programu na miradi ya hali ya hewa inayotekelezwa kwa nchi wanachama wa SADC," alisema Dk. Kijazi.

Alibainisha kwamba ni rahisi pia kupata taarifa za hali mbaya ya hewa kwa nchi wananchama ikiwemo Tanzania  na kupata ujuzi wa kimataifa.

Dk. Kijazi ambaye pia ni Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO), alisema TMA imejipanga kufikia azma ya Mwenyekiti wa SADC, Rais John Magufuli ya kuifanya Tanzania kufikia uchumi wa kati wa viwanda.

No comments:

Post a Comment

Pages