Mwenyekiti wa Club ya Waandishi wa Habari mkoani Kagera, Mbeki Mbeki (kushoto), akisalimiana na Katibu Tawala Wilaya ya Misenyi, Abdallah Mayomba.
Lydia Lugakila, Bukoba
Kauli hiyo imetolewa leo Septemba 16,
2019 na Mwenyekiti wa club ya waandishi
mkoani Kagera Mbeki Mbeki wakati
akiongea na baadhi ya waandishi wa habari wilayani misenyi mkoani Kagera
waliotaka kujua nafasi ya tasnia ya habari
katika kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa.
Mbeki amesema ni lazima waandishi wa Habari watambue kuwa
wafanya kazi chini ya sheria za nchi hivyo wanatakiwa kuepuka kuandika habari
zinazoegemea upande mmoja au habari za uchochezi ambazo haziwezi kuleta matokeo chanya katika
jamii.
Kwa upande wake katibu tawala wilayani
Misenyi Bwana Abdallah Mayomba amesema serikali wilayani humo itahakikisha
inakuwa bega kwa began a waandishi wa habari ikiwemokutoa ufafanuzi wa mambo
yatakayohitaji kuhabarisha wananchi.
No comments:
Post a Comment