Mchungaji wa Kanisa la Kinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Mtaa wa Ibura Mchungaji Gabriel Lugakingira akiongoza ibada ya Jumapili.
Na Lydia Lugakila, Bukoba
Waumini wa madhehebu mbalimbali,
viongozi wa dini na viongozi wa serikali
mkoani Kagera wametakiwa kujiadhali na matumizi
ya ndimi zao ili kuepukana na kauli
zinazoweza kusababisha migogoro isiyoisha.
Kauli hiyo imetolewa leo Septemba
8, 2019 na Mchungaji wa Kanisa la Kinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Mtaa wa Ibura Mchungaji Gabriel Lugakingira katika ibada
iliyofanyika kanisani hapo.
Mchungaji Lugakingira ameendesha ibada hiyo kwa
kuongozwa na maneno ya mungu kutoka Kitabu cha Mathayo mtakatifu 20, 20-23.
Mtumishi huyo amesema kuwa muumini
yeyote kiongozi yeyote anayetoa kauli mbovu na kashifa ni chanzo kikubwa cha
kuwepo kwa migogoro isiyoisha.
Amewataka kulifuata neno la mungu kwa
kuchunga sana mdomo unaotoa kauli na kuwa mdomo unaweza kuunganisha watu na
unaweza kufarakanisha hivyo amesisitiza
watu kujiadhali na matumizi mabaya ya ndimi zao.
‘’Dunia imeisha haribika vibaya watu
wameshindwa kutumia Ndimi zao kila muhubiri anakuja na ndimi zake kwa waumini
nyingine zikiwa za kashfa , zinazoeneza migogoro jiadhalini na mdomo tubuni dhambi mtolee mungu shukrani ‘’amesema.
Amesema ulimi huo huo umesababisha
hata kudharauliana kiimani na hata kuchochea ubnafsi
huku akitaja sehemu ya stendi za mabasi kutumia ndimi zao vibaya .
Amesema jitihada za wanadamu
zimeshindwa kuleta mafanikio dunia kutokana na ndimi zao hivyo amewahimiza
kutoka katika mitihani ya ibilisi na
kufuata mitihani ya mwenyezi mungu.
Hata hiyo katika ibada hiyo
yamefanyika maombi maalum kwa ajili ya kuwaombea wanafunzi wanaotarajia kufanya
mthihani wa Darasa la saba.
No comments:
Post a Comment