HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 08, 2019

CEED YAWAPATIA ELIMU WAJASIRIAMALI

Mjasiriamali Archad Kato kutoka Kampuni ya uzalishaji mvinyo ya Alko Vitanges, akizungumza na wafanyabishara wenzake  juu ya fursa, uzoefu pamoja na changamoto mbalimbali katika ukuzaji wa biashara. (Na Mpiga Picha Wetu).



Na Mwandishi Wetu

 
KITUO cha Ujasiriamali na Maendeleo ya Utendaji (CEED), kimeamua kuwakutanisha  wajasiriamali zaidi ya 52 kutoka sehemu mbalimbali za  jijini Dodoma na nje kwa lengo la kuwapa elimu ya usimamizi na ukuzaji wa biashara zao ndani ya jiji hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari, mwakilishi kutoka CEED Tanzania, Fred Laiser, amesema wameamua kuwakutanisha wajasiriamali hao katika semina hiyo  kwa ajili ya kuwapa ujuzi  wa namna ya kuboresha biashara zao.

Amesema pia wameamua kuwapa ujuzi wa namna ya kutafuta ushindani wa kusaka fursa mbalimbali kutokana na  kuongeza kwa idadi kubwa ya watu baada ya serikali kuhamishia shughuli zake hapa Dodoma.

‘’Sisi CEED Tanzania lengo letu kuu ni kuwasaidia wajasiriamali hapa nchini hasa katika kukuza biashara zao. Leo tupo hapa Dodoma kwa lengo kuwapa elimu na kutoa fursa mbalimbali za kibiashara ambazo wajariamali wanaweza kuzichangamkia. Pia kuwakutanisha na wenzao wajifunze namna ya kukuza biashara zao, kutatua changamoto zao.’’ amesema Laiser.

Mbali na hilo,  Laiser ametumia nafasi hiyo kuwataka wajasirimali mbalimbali nchini kujitokeza kwa wingi katika semina mbalimbali za ujasiriamali hasa zinazoendeshwa na CEED Tanzania kwaji ajili ya kupata ujuzi wa biashara zao na pia kufahamiana na wajasiriamali kutoka kila kona ya Tanzania.

Kwa upande wa wanufaikaji wa mafunzo hayo, Archad Kato kutoka Kampuni ya uzalishaji mvinyo ya Alko Vitanges, amesema mafunzo hayo ni muhimu kwao kwani yanawasaidia kujua mbinu mbalimbali za ufanyaji wa biashara.

‘’Nawapongeza sana CEED Tanzania kwa kutupa nafasi hii ya kujifunza na kukutana na wajasiriamali wenzetu ili kujifunza mambo mbalimbali kutoka kwao, moja ya changamoto inayotukabili sisi wajasiriamali hapa nchini ni kushindwa kuendeleza biashara zetu mara baada ya kuanzisha.

Wengi tunapenda kujiajiri lakini wachache ndio wanaofikia malengo yao, Ili kutatua changamoto hizi inatupasa kujifunza vitu vipya kila siku na kujaribu mara kwa mara mpaka pale biashara itakapoweza kujiendesha yenyewe ‘’.amesema  Kato.

Naye Elizabeth Swai ambaye ni  mwanzilishi wa kampuni ya ufugaji kuku ya AKM Glitters Limited, alitumia nafasi hiyo kuwataka wajasiriamali kutumia vizuri teknolojia katika kujifunza masuala mbalimbali kwasababu teknolojia imerahisisha kila kitu kwasasa.

"Ni Rahisi kupata taarifa mbalimbali zitakazowasaidia kujielimisha na kukuza biashara zetu kwa kutumia teknolojia hivyo tusiwe mbali na vitu kama hivi, " amesema.

No comments:

Post a Comment

Pages