Mkuu
wa Kitengo cha huduma kwa wateja kutoka Tigo, Mwangaza Matotola
akiongea na waandishi wa habari katika uzinduzi wa maadhimisho ya wiki
ya huduma kwa wateja.
Dar es Salaam. Oktoba 7, 2019. Kampuni inayolenga kuleta mageuzi ya kidijitali
katika maisha ya watanzania, Tigo, leo imezindua maadhimisho ya wiki ya huduma
kwa wateja kwa kutambua mchango wa watoa huduma wake katika kuhakikisha wateja wanapata
huduma zenye ubora.
Wiki
hiyo inayoadhimishwa ulimwenguni kote imebeba kauli mbiu isemayo “Magic of
Service” yaani huduma ya maajabu na imezinduliwa rasmi leo na itamalizika Oktoba 11.
Akizungumza
wakati wa hafla iliyofanyika katika Kituo cha huduma kwa wateja cha Tigo,
Meneja wa Huduma kwa wateja, Mwangaza Matotola amesema wiki hii itaadhimishwa
kwa aina yake kwa kuhimiza ubora wa huduma ili kuendana na mahitaji ya wateja.
“Huduma
kwa wateja ni kitovu cha biashara yetu na ndiyo maana tunaweka kipaumbele
katika kuhakikisha wateja wanapata huduma zenye ubora na weledi siku zote hivyo
katika wiki hii tumejizatiti kuhimiza dhamira yetu ya kutoa huduma zenye
kukidhi mahitaji ya wateja,” alisema Matotola.
Wiki
hiyo itaambatana na matukio mbalimbali ikiwamo kutembelea kituo cha huduma kwa
wateja, kujumuika na wateja pamoja na wadau ili kujadili namna bora zaidi ya
kuendeleza huduma za kampuni hiyo.
Meneja
huyo aliwahimiza wateja kutumia huduma mbalimbali za kimtandao kama WhatsApp,
Twitter, Facebook na Instagram pale wanapohitaji huduma au msaada kutoka kwa
wataalamu wenye weledi.
“Tigo
imeendelea kuwekeza katika kuboresha huduma kwa kutoa mafunzo kwa wafanyakazi
wetu na zaidi tumewekeza zaidi katika kujenga miundombinu ya kituo chetu cha
mawasiliano ili kuhakiisha wateja wanapata huduma za uhakika,” alisema
Aidha,
wiki hiyo itahitimishwa kwa kutoa tuzo kwa mfanyakazi bora wa mwaka ambaye
ameonesha weledi mkubwa katika utoaji wa huduma ikiwa ni njia ya kutoa hamasa
kwa wafanyakazi wengine.
No comments:
Post a Comment