HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 28, 2019

CRDB yaimwagia sifa Fountain Gate Academy

 Mchezaji bora wa mashindano, Shaban Miyanga, akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulamajid Nsekela.
  Kukabidhi zawadi.
Kocha Bora wa mashindano, Abubakari Ally, akimuonesha tuzo aliyopata Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Fountain Gate Academy, Japhet Makau, akimkabidhi picha ya kumbukumbu ya kikosi cha timu ya Fountain Gate Academy, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulamajid Nsekela.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Fountain Gate Academy, Japhet Makau, akifafanua jambo.
 Meneja wa Fountain Gate Academy, Fred Tchalewa, akizungumza katika hafla hiyo.
Wachezaji wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, akipeana mkono na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Fountain Gate Academy, Japhet Makau. Kushoto ni Ofisa Mkuu wa Biashara Benki ya CRDB, Joseph Witts.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, akizungumza na wachezaji na viongozi wa timu ya Fountain Gate Academy walipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaa Oktoba 28, 2019.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, akizungumza na wachezaji na viongozi wa timu ya Fountain Gate Academy walipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaa Oktoba 28, 2019.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, akizungumza na wachezaji na viongozi wa timu ya Fountain Gate Academy walipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaa Oktoba 28, 2019.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, akizungumza na wachezaji na viongozi wa timu ya Fountain Gate Academy walipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaa Oktoba 28, 2019.
Mataji waliyoshinda. 
Baadhi ya viongozi wa Benki ya CRDB pamoja na wachezaji wa timu ya Fountain Gate Academy.
 Baadhi ya wachezaji wa timu ya Fountain Gate Academy.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, akizungumza na wachezaji na viongozi wa timu ya Fountain Gate Academy walipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaa Oktoba 28, 2019.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, akifafanua jambo wakati akizungumza na wachezaji wa timu ya Fountain Gate Academy walipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaa Oktoba 28, 2019.
 Baadhi ya wachezaji wa timu ya Fountain Gate Academy wakiwa katika ofisi za Benki ya CRDB jijini Dar es Salaa Oktoba 28, 2019.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, akizungumza na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Fountain Gate Academy, Japhet Makau.  
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB (katikati), akiwa katika picha ya pamoja wachezaji wa timu ya Fountain Gate Academy walipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam Oktoba 28, 2019.
 

Na Mwandishi Watu

BENKI ya CRDB imeimwangia sifa timu ya Soka ya Fountain Gate Academy ya jijini Dodoma kwa kuibuka washindi wa pili wa mashindano ya wazi ya JMK (JMK Open Tournament 2019, U17, yaliyofanyika katika dimba la JMK Park jijini Dar es Salaam.

Mashindano hayo yalihitimishwa Oktoba 27, 2019 kwa JKU ya Zanzibar kuibuka mabingwa, mashindano ambayo yalishirikisha timu nane kutoka mikoa ya Morogoro, Dodoma, Dar es Salaam na Zanzibar.

Katika mashindano hayo yaliyolindima kwa siku nne kuanzia Oktoba 24 hadi 27, Fountain Gate walidhaminiwa na Benki ya CRDB, kwa maana ya vifaa vya michezo na mahitaji madogo madogo.

Licha ya kupoteza pambano hilo la Fainali Fountain walizadiwa kikombe cha mshindi wa pili ambacho jana walikikabidhi kwa wadhamini wao Benki ya CRDB kupitia kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Abdulimajid Nsekela.

Nsekela aliwapongeza kwa kuiwakilisha vyema nembo CRDB katika mashindano hayo, huku akiwataka kuongeza juhudi zaidi katika kuendeleza vipaji vyao kwa ustawi wa maendeleo yao.

"Nianze kwa kuwapongeza Uongozi, Kocha na Wachezaji wa kwa kazi nzuri mliyoifanya kwenye mashindano ambayo mmeshiriki kwa mara ya kwanza lakini kwenda mpaka fainali mmewashinda wengi.

"Lakini naomba niwapongeze kipekee kwa kutangaza nembo yetu vizuri, tulikuwa tunaangalia picha kwenye magazeti, mitandao ya kijamii, kila tulipowaangalia tulikuwa tunaiona CRDB,"alisema Nsekela na kuongeza kuwa.

"Pia nitumie fursa hii kuushukuru Uongozi kwa kutambua kuja kutoa shukrani, maana sio wote huwa wanarudi kutoa mkono wa asante."

Lakini pia alitoa ushauri kwa Uongozi wa Fountain kuimarisha timu zao za U 13na U 15 kwani ndio zinatengeneza U 17 imara huku akiahidi kuendeleza ushirikiano kwa taasisi hizo mbili.

"Imani yetu vijana hawa kama wataendelea kuwekewa mazingira mazuri ya kuvitumua vipaji vyao ndio wachezaji wa Timu ya Taifa ijayo. Sisi kama CRBD siku zote tunapenda kushirikiana na taasisi au watu waliofanikiwa kama sisi.
Kwa upande wa Nahodha wa Timu ya Fountain Gate Academy Amani Jonas, " alisema wazazi wasiwabanie watoto kujihusisha na michezo ili kuweza kufikia mafanikio yao binafsi.

Pia Jonas alifunguliwa akaunt ya CRDB na kuwekewa akiba ya sh 200,000. kama zawadi kwa kuingoza timu yake kufanya vizuri kwenye mashindano hayo.
"Najisikia furaha sana, sikuwahi kuwaza kuwa ntakuja kuwa na akaunti yangu ya benki lakini leo nimefunguliwa kutokana na kipaji changu. Nawashauri wazazi wasiwabanie watoto wao kufanya kitu ambacho wanakipenda," alisema Jonas.

No comments:

Post a Comment

Pages