Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda leo Oktoba 9 amezindua mfumo
wa kuwawezesha wananchi wa Mkoa huo kuwasilisha kero na changamoto
walizonazo kwa kutumia simu ya mkononi au Computer na ujumbe wao
kuwafikia watendaji kwa haraka na kupatiwa majibu ndani ya muda mfupi
jambo litakalosaidia kuokoa Muda na gharama za usafiri.
RC
Makonda amesema ameamua kuanzisha mfumo huo baada ya kubaini kuwa
wananchi wengi wamekuwa wakifika kwenye ofisi za umma na kupewa majibu
ya "Njoo Kesho" pasipokujua kuwa wamepoteza muda na nauli zao kufuata
huduma.
Aidha RC Makonda
amebainisha kuwa mfumo huo utakuwa ukipokea taarifa za malalamiko ya
Watendaji wasiowajibika kuanzia ngazi ya Mtaa, Kata, Wilaya hadi Mkoa na
taarifa zitawafikia Viongozi wote kuanzia RC Makonda mwenyewe, Mkuu wa
Wilaya husika, Mkurugenzi, Katibu tawala na Mkuu wa idara.
Hata
RC Makonda amewahimiza wananchi kutumia mfumo huo kueleza kero zote
zinazowakabili ikiwemo Afya, Barabara, Elimu, Maji, Umeme, Miradi
inayokwama pamoja na kutoa taarifa pindi wanapobaini uhalifu kwenye
mtaa.
Jinsi kuwasilisha ujumbe andika neno DSM kisha eleza changamoto zako kisha tuma kwenye namba 11000 au ingia kwenye Website www.malalamiko.dsm.go.tz na ujumbe wako utapokelewa mara moja na kupewa mrejesho
No comments:
Post a Comment