HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 03, 2019

NMB YAZINDUA WIKI YA HUDUMA KWA MTEJA YENYE KAULIMBIU UBORA UKO HAPA

Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Sipora Liana (wa pili kushoto), akimkabidhi cheti mteja wa Benki ya NMB, Lucas Bise, wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Mteja uliofanyika katika Tawi la Mlimani City jijini Dar es Salaam. Katikati ni Meneja wa tawi hilo, Irene Masaki. Anayeshuhudia kushoto ni Ofisa Mkuu wa Fedha wa NMB, Ruth Zaipuna. (Picha na Francis Dande).

 Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Mlimani City, Irene Masaki, akizungumza na wateja katika hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Mteja.
 Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd akizungumza katika hafla hiyo.
Ofisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja.
 Baadhi ya wafanyakazi na wateja.
 Wateja waliohudhuria hafla hiyo.
Baadhi ya waandishi wa habari.
 Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Sipora Liana, akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Mteja iliyofanyika katika Tawi la NMB Mlimani City.

 Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd, akimpongeza Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Sipora Liana, baada ya kutoa hotuba yake.

 Mmoja wa wateja wa Benki ya NMB akizungumza katika hafla hiyo.
 Mgeni rasmi akiwa katika picha ya viongozi wa Benki ya NMB pamoja na Benki ya NMB.

Picha ya pamoja ya wafanyakazi wa NMB.
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Sipora Liana, akikata keki na  Ofisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna (kushoto). 


NA MWANDISHI WETU
BENKI ya NMB jana imezindua Wiki ya Huduma kwa Mteja Duniani, huku ikiahidi kuitumia fursa hiyo kuzungumza na wateja kuhusu mipango na maboresho mbalimbali ya kihuduma na kwamba ubora wa huduma zao ni endelevu na sio kwa wiki hiyo pekee.

Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam jana na Ofisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, mbele ya Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Spora Liana, ambaye alikuwa mgeni rasmi wa hafla ya uzinduzi huo iliyofanyika katika Tawi la NMB Mlimani City.

Zaipuna alisema kuwa, chini ya kaulimbiu ya wiki hiyo kwa NMB - isemayo ‘Ubora Uko Hapa,’ watapokea na kuyafanyia kazi maoni ya wateja wao.

“Ni wiki ambayo tunazungumza na wateja kuwaeleza mipango na maboresho mbalimbali ambayo tunaendelea kufanya, pia kupokea maoni yao, lengo ni kuonesha kwamba tunamjali mteja wetu na kumsogezea huduma karibu kabisa na mahali alipo,” alisema.

Wiki ya Huduma kwa Mteja Duniani ilianza Oktoba Mosi duniani kote, lakini Zaipuna akasisitiza kuwa kwao NMB wataitumia wiki hiyo kutoa elimu juu ya umuhimu wa huduma bora na rafiki kwa wateja, lakini pia kuelimisha wateja wao juu ya umuhimu wa watoa huduma.

Aliongeza ya kwamba, ushindi wa miaka saba mfululizo wa Tuzo ya Benki Bora Tanzania inayotolewa na Jarida la Euromoney na uwepo wa tawi la NMB kwa kila wilaya, ni uthibitisho wa ubora wa huduma na ongezeko la wateja (kutoka 600,000 mwaka 2005 hadi milioni 3.5).

Kwa mujibu wa Zaipuna, NMB haikuwa na mashine za kutolea fedha (ATM) miaka 14 iliyopita, lakini leo ina mashine hizo zipatazo 800, ambazo ni sawa na asilimia 40 ya ATM zote zilizopo Tanzania. Pia benki haikuwa na Wakala wa Huduma za Kibenki wakati huo, lakini sasa ina NMB Wakala zaidi ya 7000.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Spora Liana, aliipongeza NMB kwa kutimiza kwa vitendo Kaulimbiu ya NMB Karibu Yako na kwamba kauli hiyo haijawalenga wateja wao tu, bali jamii ya nzima ya Kitanzania kutokana na sapoti za benki hiyo kwa jamii.

“Mmethibitisha kuwa Kweli NMB Karibu Yako. Hili mmelipa uzito na thamani sawa sio tu kwa wateja wenu, bali hata kwa jamii, mkiwa vinara wa usaidizi wa changamoto za kielimu, kiafya na majanga yanayoikumba jamii. Mmetoa kwa nyakati tofauti vifaa tiba, vifaa vya elimu nk,” alisema Spora.

Alienda mbali zaidi kwa kuitaka NMB kuhakikisha inajiandaa kuingia na kutoa huduma katika Stendi Mpya ya Mabasi ya mikoani na nje ya nchi inayojengwa Mbezi Louis, ambako kutakuwa na ofisi mbalimbali za kutoa huduma za fedha kwa wageni wa ndani na nje ya nchi watakaoingia jijini.

Sambamba na hilo, Spora aliiomba NMB kujipanga kuhakikisha inatumia fursa ya mchakato wa Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam wa kuibadili Kariakoo kuwa ‘Dubai ya Tanzania’ kwa huduma za kibiashara saa 24, ili waweze kutoa huduma za kifedha kwa saa nyingi zaidi nyakati za usiku.

No comments:

Post a Comment

Pages