HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 05, 2019

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA HOSPITALI YA HALMASHAURI YA MJI WA TUNDUMA PAMOJA NA UJENZI WA BARABARA YA MPEMBA-ISONGOLE KM 50.3 TUNDUMA MKOANI SONGWE

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe pamoja na Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo ili kuweka jiwe la msingi ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Tunduma katika eneo la Mpemba Tunduma mkoani Songwe.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua sehemu ya majengo ya Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Tunduma katika eneo la Mpemba Tunduma mkoani Songwe.
 Ujenzi wa majengo ya Hospitali ya Halmashauri ya Mji
wa Tunduma katika eneo la Mpemba Tunduma mkoani Songwe ukiwa katika hatua za mwisho.
 Mfano wa hospitali hiyo ya Halmashauri ya Mji wa
Tunduma utakavyokuwa mara baada ya kukamilika.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe pamoja na Viongozi wengine kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa barabara ya Mpemba-Isongole km 50.3 itakayojengwa kwa kiwango cha lami.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mtoto Joan Schinga mmoja wa wanakwaya ya Watoto ya Light Angels ya Kanisa la Moravian Tunduma ambao waliimba wimbo wa kukemea Rushwa mara baada ya uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa barabara ya Mpemba-Isongole km 50.3 itakayojengwa kwa kiwango cha lami.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Mbozi wakati akielekea Mpemba mkoani Songwe.
Wanakwaya ya Light Angels ya Kanisa la Moravian
Tunduma mkoani Songwe wakiimba wimbo maalum wa kukemea Rushwa katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa barabara ya Mpemba-Isongole km 50.3 itakayojengwa kwa kiwango cha lami.
PICHA NA IKULU.

No comments:

Post a Comment

Pages