Sensei
Abdallah Kambi enzi za uhai wake.
NA
MWANDISHI WETU
MKUFUNZI na Mkuu wa Idara ya Ufundi ya JKA/WF Tanzania kitaifa,
pia Mwenyekiti wa Tanzania Shotokan Ryu Karate Do Association (TASHOKA), Sensei
Abdallah Kambi, amefariki Dunia.
Sensei Kambi aliyeingia madarakani Julai 27, 2019, amefikwa
na umauti jana alfajiri katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, alipokuwa amelazwa
kufuatia kusumbuliwa na kifua na tumbo, tangu Agosti mwaka huu.
Mwenyekiti wa JKA/WF Tanzania, Jerome Mhagama, amethibitisha
kutokea kwa msiba huo na kwamba Sensei Kambi ambaye alijiunga na JKA/WF Tanzania
mwaka 2009 na kuwa mwanafamilia hai mpaka umauti unamkuta.
Katika hatua nyingine, Mhagama alisema taarifa zaidi za msiba
wa mdau huyo wa mchezo wa Karate, wanasubiri majibu ya kikao cha familia ya
marehemu.
“Ndani ya JKA, Kambi Sensei alikuwa mmoja wa Wakufunzi
tegemezi mwenye Mkanda Mweusi Dani 4 ‘Black Belt 4th Dan-‐JKA’, pia alikuwa na
leseni ya kimataifa ‘JKA International License’ yenye viwango vya ‘Instructor
class C’, ‘Judge class D & Examiner class D’”, alisema Mhagama katika
taarifa yake kwa vyombo vya habari jana.
Mungu ailaze mahala pema roho ya maremu. Bwana ametoa, Bwana
ametwaa, jina lake lihimidiwe.
Alale mahali pema peponi..!
No comments:
Post a Comment