HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 10, 2019

TMA kutoa mwelekeo wa mvua za miezi sita

Na Irene Mark

LICHA ya mvua nyingi zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam na maeneo ya baadhi ya mikoa ya nchi, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), leo Oktoba 10,2019 itatoa mwelekeo wa mvua za vuli.

Taarifa kutoka TMA zinataja pamoja na Dar es Salaam mikoa ambayo mvua zinaendelea kumuesha ni Pwani, Mtwara, Lindi, Tanga na Kaskazini mwa Morogo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ni utaratibu wa kawaida wa TMA kukutana na wadau wakiwemo wanahabari kujadili na kuoneshwa namna mvua mwaka zinavyoenda.

"Kesho (leo), tutatoa mwelekeo wa mvua za mwaka zinazonyeesha kwa miezi sita kuanzia Novemba mwaka huu hadi Aprili,2020 na hizi zinanyeesha kwenye baadhi ya mikoa," alisema Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Agnes Kijazi  wakati wa semina ya Wanahabari jana Oktoba 9, 2019.

No comments:

Post a Comment

Pages