KAIMU
Ofisa Mkuu wa Idara ya Wateja wakubwa wa Benki ya NMB, Aziz Chacha,
akizungumza na baadhi ya wateja wa benki hiyo (hawapo pichani) wakati wa
Hafla ya Jukwaa la Wafanyabiashara Wakubwa lililofanyika leo jijini Dar es Salaam.
NA SALUM MKANDEMBA
BENKI
ya NMB imewahakikishia wateja wakubwa nchini huduma bora na timilifu kulingana
na mahitaji yao ya kifedha, uhakika unaotokana na ukubwa wa mtaji wa benki hiyo
unaofikia zaidi ya Sh. Bilioni 700.
Hayo
yalisemwa jana na Kaimu Ofisa Mkuu wa Idara ya Wateja Wakubwa wa NMB, Aziz
Chacha, wakati akifungua Jukwaa la Wateja Wakubwa (NMB Executive Network), lililofanyika
leo jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma.
Muro
alibainisha ya kwamba, uwezo wa kipesa unaotokana na ukubwa wa mtaji katika
benki ya NMB ni mkubwa, unaowawezesha kuhudumia wateja wa kada zote, wakiwamo
wateja wakubwa na kumudu kwa asilimia zote mahitaji yao ya kifedha.
Aliongeza
ya kwamba wateja wakubwa wana mahitaji makubwa ya kihuduma, lakini wao wana
nguvu ya kutosha kuyatimiza na ndio maana wakawaalika katika jukwaa hilo, ili
kujadiliana kwa pamoja kujua namna ya kushughulika na changamoto zao na
kuzitatua.
Kwa
upande wake, Meneja Uhusiano wa Kitengo cha Wateja Wakubwa wa NMB, Amour Muro, alisema
NMB Executive Network ni jukwaa linalotumika kukutana
na wateja wakubwa, ikiwa ni sehemu ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.
“Hili
ni moja ya majukumu yetu katika wiki hii na hii inatusaidia kuzungumza nao
kujua namna ya kuongeza thamani ya huduma tunazowapatia. Kupitia Jukwaa kama
hili, tunatanua uelewa na kuongeza thamani ya kupitia majadiliano tutakayofanya,”
alisema Muro.
Alisema
NMB kama taasisi inaamini katika huduma walizonazo, lakini njia bora na sahihi
ya kuzifanyia maboresho mbalimbali ni kukutana na makundi tofauti ya wateja,
kusikiliza changamoto zao na kuzifanyia kazi, ili kuwezesha upigaji hatua za
maendeleo yao.
Magdalena
Magali, ambaye ni mwakilishi wa Kampuni ya Saruji ya Tanzania Potland, kwa
upande wake aliishukuru NMB kwa kuwaandalia jukwaa maluum wateja wakubwa na
kupokea mawazo yao chanya kwa maendeleo ya mtu mmoja mmoja, wateja na taasisi
hiyo kwa ujumla.
Aliipongeza
NMB kwa mabadiliko chanya ya kimfumo kutoka analogi kwenda dijitali, uliojikita
katika kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa haraka, wepesi na usalama na
kuwataka Watanzania kuchangamkia huduma hizo ili kuokoa muda na kwenda na
wakati.
Naye
Steven Gideon, ambaye ni Ofisa Mipango na Bajeti wa Kampuni ya Simu Tanzania
(TTCL), alisema kampuni yake inapongeza uamuzi wa NMB kukutana na kujadiliana
nao, kwani njia rahisi ya kufikia malengo ni kufanyia kazi changamoto zilizopo
ilikusonga mbele.
Gideon
aliwataka Watanzania kujali muda na kuendana na kasi za maendeleo kwa kuchagua
kuifanya NMB kuwa mshirika sahihi wa ukuaji kiuchumi na kwamba siri ya
mafanikio iko katika mapinduzi ya kiteknolojia yaliyofanywa na benki hiyo,
yanayoongeza ufanisi kwa wateja.
No comments:
Post a Comment