Mwenyekiti wa Chadema
Ubungo, Idan Msuya (kulia), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu zoezi la uchukuaji na urudishaji fomu za kugombea uchaguzi wa serikali za mitaa. (Picha na Tatu Mohamed).
NA TATU MOHAMED
NA TATU MOHAMED
CHAMA
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jimbo la Ubungo kimelalamikia
kufanyiwa figisufigisu katika zoezi la uchukuaji na urudishaji fomu za
kugombea uchaguzi wa serikali za mitaa ambalo limemalizika leo.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Chadema
Ubungo, Idan Msuya, amesema yapo maeneo ambayo wamebaini kuwekwa majina
hewa huku wasimamizi wakigoma kuwasikiliza.
Amesema Mtaa wa Msewe wameongeza majina ya watu hewa 400 na mitaa mingine na kwamba ushahidi wanao.
"Watu
hao wameongezwa kwa lengo la kujihami ili kumfurahisha Rais John
magufuli kuwa wameandikisha watu wengi kumbe kiuhalisia sio kweli.
"Yaani
tunashangazwa kufanyiwa figisu katika mchakato wa uchaguzi wa serikali
za mtaa wakati tuna miaka minne hatujawahi kufanya kampeni za chama
wala mikutano," amesema.
Aidha amesema wasimamizi walikuwa wakali katika utoaji wa fomu na ukionekana unadai kwa nguvu unaitiwa polisi.
“Katika
hizi fomu kuna kipengele namba C mpokeaji anaposwa kupokea fomu kutia
saini, kuweka mhuru na kuonyesha kuwa fomu ameipokea saa ngapi mbele ya
yule aliyerejesha fomu kwenye mitaa mingi ya Ubungo hilo halijafanyika
hata tulivyowaomba nakala ya fomu waligoma kuzitoa.
"Nilivyopiga
simu kwa mmoja wa wasimamizi alinijibu kuwa kwa sasa wametoa maelekezo
zisitolewe hizo fomu wala kusaini hadi Novemba 5, 2019 jambo ambalo
lipo nje ya utaratibu. Utaratibu unamtaka mgombea asitoke bila kupatiwa
nakala hicho kitendo kinaacha mianya ya kufanyia uovu katika zoezi a
urejeshaji wa fomu,” amesema.
Msuya
amesema kitendo cha mgombea wake kuondoka bila fomu ya kuonyesha kuwa
amerejesha fomu ina maana wanaweza kuambiwa mgombea hakurudisha fomu kwa
muda unaotakiwa.
Ameongeza kuwa kuna Kata zimetumika fomu za kughushi zikionyesha zimegongwa mhuri wa kata wakati sio kweli
No comments:
Post a Comment