Naibu Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi
na Usalama mkoani Simiyu, alipowasili leo kwa ziara ya kikazi inayohusu Jeshi
la Magereza mkoani humo kuanza kilimo cha pamba kwa kutumia ardhi na nguvukazi
ya wafungwa walionao.Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka. (Picha
na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Naibu Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati),akitoka kuzungumza na
mahabusu waliohifadhiwa katika Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Busega,mkoani
Simiyu.
Na Mwandishi Wetu,
Simiyu
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka amelitaka Jeshi la
Magereza kutumia jumla ya Ekali Elfu Tatu na Sabini na Moja zilizopo mkoani hapo kwa kilimo cha pamba
ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Dkt.John Magufuli la kutaka jeshi hilo
kubadilika na kuingia kwenye mfumo wa uzalishaji ili liweze kuondokana na mfumo
wa kutegemea bajeti kuu ya Serikali kulisha wafungwa nchini.
Ameyasema hayo wakati
wa ziara ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni mkoani
hapo lengo ikiwa ukaguzi wa shughuli za taasisi zilizopo chini ya wizara hiyo
na kuangalia fursa zinazopatikana katika mikoa mbalimbali nchini ili kuweza
kulibadilisha jeshi la magereza
“Mheshimiwa naibu waziri sisi kama mkoa tuko tayari kushikana
na jeshi la magereza kwani kuna ardhi ya kutosha na naomba nikuhakikishie hawa
wakilima pamba japo ekali mia moja tu na zikauzwa wataweza kufanya mambo mengi
ya maendeleo ikiwemo kujenga nyumba za kuishi askari ambazo zitakua ni za
kiwango cha juu,” alisema Mtaka
Akizungumza katika ziara hiyo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani
ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni alisema Serikali imelipokea jambo hilo kwani
ndio lengo hasa la serikali kuona jeshi la magereza linajitegemea katika
uendeshaji wake pasipo kutegemea bajeti kuu ya serikali
“Mheshimiwa Rais alishatuagiza tulibadilishe jeshi hili la
magereza na tayari tushaanza na tumetenga magereza kumi ya kimkakati nchini
ambayo yameteuliwa kuleta mapinduzi katika jeshi, ziara hii ni kuona fursa
zilizopo katika mikoa mingine kupitia magereza,nakuahidi jambo hilo
tumelichukua kama wizara na muda si mrefu litapatiwa ufumbuzi,” alisema Masauni
Naibu Waziri Masauni pia alipata nafasi ya kutembelea Kituo
cha Polisi cha Wilaya ya Busega na kuzungumza na mahabusu waliopo kituoni hapo
ambapo akuridhishwa na hali ya uchafu katika chumba cha mahabusu kituoni hapo
na kuuagiza uongozi kufanya utaratibu wa kusafishwa kwani waliopo ndani ni
binadamu na wana haki zao ikiwepo kukaa sehemu safi ili kulinda afya zao.
No comments:
Post a Comment