NA
TIGANYA VINCENT
SERIKALI
imeahidi kutoa kutoa milioni 300 kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa usambazaji wa
maji kwa wananchi kutoka chanzo cha maji cha Tura wilayani Uyui ili kuwaondolea kero ya upatikanaji wa maji ya
uhakika ya muda mrefu kwa wakazi wa eneo hilo.
Fedha
hizo ni sehemu zitakazotumika katika kukamilisha mradi huo ndani ya kipindi cha miezi mitatu.
Kauli
hiyo imetolewa leo na Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa wakati wa ziara
yake Wilayani Uyui Mkoani Tabora kwa ajili ya kutatua kero za maji kwa wananchi
wa eneo hilo.
Alisema
kukamilika kwa chanzo hicho cha maji kitasaidia kuzalisha lita zaidi ya milioni
2.7 na kuwahudumia wakazi zaidi ya 11,000 na hivyo kuwaondolea usumbufu wa
kutembea umbali mrefu kutafuta maji.
Alisema
kuwa Serikali haiwezi kuona wananchi wanateseka kutafuta maji kwa umbali mrefu
huku kukikwa na chanzo cha maji kizuri ambacho hakitumiki.
Waziri
huyo alisema mradi huo utakuwa na hatua tatu ambazo ni ujenzi wa kituo cha
kutoa maji kwenye bwawa na kusafisha maji, hatua ya pili ni ujenzi wa
tenki la
upokeaji wa maji na hatua ya
mwisho ni ujenzi wa miundombinu ya usambazaji wa maji kwa wananchi.
Naye
Mbunge wa Jimbo Igalula Mussa Ntimizi alisema kuwa licha ya bwawa hilo kumilikiwa
na Shirika la Reli Tanzania(TRL) wamekubaliwa lianze kutumika kutatua kero ya
maji kwa wananchi
No comments:
Post a Comment