Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo Dk. Respicious Boniface, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani).
Na Asha Mwakyonde
TAASISI ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI), imewafanyia upasuaji mbali mbali wa kibingwa wagonjwa 43,200 katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais John Magufuli
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Novemba 22, 2019 wakati akielezea mafanikio ya MOI kwa kipindi cha miaka minne ,Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo Dk. Respicious Boniface amesema kuwa gharama za matibabu hayo ndani ya nchi zilikua Shilingi za Kitanzania bilioni 16.5.
Mkurugenzi huyo amefafanua kwamba wagonjwa hao kama wangepelekwa nje ya nchi kwa matibabu jumla ya shilingi bilioni 54.9 zingetumika..
Amefafanua kuwa tasisi hiyo imeokoa shilingi bilioni 38.4, ambazo zitatumika kwa shughuli nyingine za maendeleo ya nchi.
Huduma mpya zilizoanzishwa hapa MOI katika kipindi hiki.
Amesema kuwa upasuaji huo umefanyika kwa wagonjwa wa Kubadilisha nyonga 900
Kubadilisha magoti 870
, upasuaji wa mfupa wa kiuno 618 upasuaji wa Ubongo 880 na watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi 2,070.
"Maboresho haya yamesaidia Taasisi ya MOI kuendelea kuboresha huduma za matibabu ya kibingwa ya Mifupa, Ubongo, Uti wa mgongo na Mishipa ya Fahamu, na hivyo kuokoa maisha ya Watanzania wengi na pesa za serikali ambazo zingetumika kupeleka wagonjwa nje ya nchi kwa matibabu,"amesema.
Amesrma serikali ya awamu ya Tano, Ilitoa shilingi bilioni 16.5 kwa ajili ya kukamilisha mradi wa jengo jipya la MOI (MOI Phase III) na kununua vifaa tiba vya kisasa.
Mkurugenzi huyo amesema miundo mbinu hiyo imesaidia kuongeza idadi ya wagonjwa wa upasuaji kutoka 400 - 500 kwa mwezi hadi 700 - 900 kwa mwezi.
Amesema idadi ya vitanda imeongezeka kutoka vitanda 150 hadi vitanda 340 vya wagonjwa wa kawaida (Public Patients) na kwamba hakuna mgonjwa anayelala chini kstika taasisi hiyo.
Dk. Boniface amesema mafanikio mengine ni kuongezeka kwa vitanda vya wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (Intensive Care Unit) kutoka vitanda 8 hadi 18 na kuanzishwa kwa chumba cha High Dependency Unit kutoka kitanda 0 hadi vitanda 16. Kuongeza vyumba vya upasuaji kutoka 6 hadi 9.

No comments:
Post a Comment