NCHI
za Kusini mwa Jangwa la Sahara na Afrika kwa ujumla zimeshauriwa kuwekeza
kwenye shughuli za utafiti ili kurahisisha utatuzi wa changamoto zinazokabili
nchi na wananchi.
Ushauri
huo umetolewa na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Baraza la Sayansi Kanda ya Afrika ulionza
Novemba 11 hadi 15 jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
na waandishi wa habari baada ya mkutano huo kumalizika, Mkurugenzi Mkuu wa Tume
ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dk. Amos Nungu (pichani), alisema umekuwa na
mafanikio makubwa kwa kada ya sayansi na utafiti kwa Ukanda wa Kusini mwa
Jangwa la Afrika.
Alisema
washiriki walisisitiza uwekezaji kwenye utafiti kama nyezo muhimu ya kuchochea
maendeleo ya nchi na wananchi.
Dk.
Nungu alisema utafiti unapaswa kuchukuliwa kwa uzito na sio maonesho, hivyo ili
hali hiyo itokee ni lazima nchi hizo kuwekeza vya kutosha.
“Tunahitaji uwekezaji na ushirikiano wa sisi
watafiti kutoka Ukanda huu wa Kusini mwa Jangwa la Afrika ili kuepuka ufanyaji
utafiti unaolenga tamanio la mfadhili na sio mahitaji ya jamii zetu,”alisema.
Alisema
uwekezaji katika eneo hilo utaondoa utafiti wa kimkakati hali ambayo itamaliza changamoto
za kijamii ambazo zinaibuka kila mara.
“Ili
kumthibitishia mwananchi kuwa ugonjwa wa kipindupindu unachangiwa na uchafu
unahitaji utafiti na sio kwenda kwa mganga wa kienyeji hivyo basi eneo hilo
linahitaji uwekezaji mkubwa kuweza kubadilisha mitazamo hiyo,” alisema.
Mkurugenzi
huyo alisema pamoja na uwekezaji kufanyika ni lazima serikali husika kuwa
tayari kutekeleza matokeo ya utafiti na sio kufungua kabatini.
Aidha,
Dk. Nungu alisema mkutano huo ambao ulikuwa na vikao vikubwa viwili na vidogo
vitano ulisisitiza kuwepo na sayansi shirikishi na wazi kama moja ya mbinu ya
kurahisha utafiti.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti Afrika Kusini (NRF), Dk. Molapo
Qhobel alisema mkutano huo umekuwa na mafanikio makubwa kwa watafiti na nchi
wanachama.
Dk.
Qhobel alisema wanasayansi watafiti ndio wanaweza kutatua changamoto ya
chakula, maji, afya, elimu na nyingine kupitia utafiti watakaofanya kila mtu
kwa lugha yake.
“Sisi
tunazungumza lugha tofauti lakini matatizo yetu yanafanana hivyo tunapaswa
kufanya kazi kwa pamoja ili kuondoa changamoto zetu kama watafiti,” alisema.
Mkurugenzi
huyo wa NRF alisema watafiti walioshiriki mkutano huo wameonesha dhamira ya
kushirikiana kuhakikisha kuwa wanakuwa kiungo muhimu kuchangia maendeleo ya
nchi na jamii zao.
Alisema
iwapo watashindwa kutumia taaluma zao kutatua changamoto za jamii elimu
waliyoipata itakuwa haina faida kwa jamii na kwao.
No comments:
Post a Comment