Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli amebatilisha
pendekezo la kufutwa shamba lenye ukubwa wa ekari 1,000 lililopo
Kidunda wilayani Mvomero mkoani Morogoro linalomilikiwa na Rusimbi.
Uamuzi
wa Dk. Mafuli kubatilisha ufutaji shamba hilo unatokana na kubainika
kuwa pendekezo lililowasilishwa la kufutwa shamba hilo kwa madai ya
kutoendelezwa kutokuwa za kweli na ulilenga kumdhulumu mmiliki wake.
Akitangaza
uamuzi huo wa Raisi jana wilayani Mvomero, Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi William Lukuvi alisema, baada ya kufuatilia mashamba
yaliyopendekezwa kufutwa Dkt Magufuli alibaini taarifa alizopelekewa za
kufuta shamba Cecilia hazikuwa sahihi na hivyo kuamua kubatilisha
pendekezo lililowasilishwa kwake na kumpatia haki yake mmiliki.
Kufuatia
hali hiyo Waziri Lukuvi aliwaonya maafisa ardhi nchini kuhakikisha
wakati wa kufanya zoezi la ukaguzi/Upekuzi wa mashamba yasiyoendelezwa
wanazingatia haki pamoja na kufuata sheria badala ya kufanya kazi hiyo
kwa upendeleo au kumuonea mtu.
Kwa
upande wake Cecilia George Rusimbi alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa uamuzi wake wa kubatilisha ufutaji sahamba
lake na kuuelezea uamuzi huo kuwa umezingatia haki na kusikia kilio chake
ambapo alisema umempa faraja baada ya kuhangaika sana kuhusiana na shamba hilo.
‘’
Nimemiliki shamba tangu mwaka 1987 na kuhangaikia hati kwa muda mrefu na
nimeshangazwa kuelezwa kuwa shamba langu liko katika mpango wa kufutwa kutokana
na kutoendelezwa, hii imenifanya kuishi kwa wasiwasi’’ alisema Cecilia.
Waziri
Lukuvi ameagiza shamba hilo la kilimo cha Michikichi, Mitiki na Bamboo
kupangwa upya na mmiliki wake kupatiwa hati kulingana na upimaji
utakaofanywa na kumtaka kuliendeleza kwa mujibu wa sheria.
Sambamba
na sakata la shamba la Cecilia, Lukuvi aliagiza kupunguzwa ukubwa wa Shamba
Sangasanga na Lubango lililodaiwa kuwa na ukubwa wa ekari 1,103 wakati uhalisia
wa shamba hilo ni ekari 500 na kuagiza mmiliki wake kurudisha hati ili apatiwe
hati ilinayolingana na uhalisia wake na ekari 603.5 zilizoongezwa zitabaki kuwa
ardhi ya akiba.
No comments:
Post a Comment