NA FARAJA EZRA
TANZANIA imewapatia Uraia zaidi ya wakimbizi 200,000 wakiwemo wazazi
na watoto huku ikiwahifafhi zaidi ya wakimbizi wapatao 330,755 hadi kufikia
Octoba 31 mwaka 2018.
Akizungumza jijini Dar es Salaam katika kilele cha
maadhimisho ya siku ya takwimu Afrika Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Philip
Mpango, alisema Tanzania ni miongoni mwa nchi inatoa misaada mikubwa kwa
wakimbizi nchini.
Dk. Mpango alibainisha kuwa miongoni mwa nchi zilizohifadhiwa
ni pamoja na Burundi ikiwa na watu 245,964 na DRC 84,170 na wengineo kutoka
nchi 15 kutoka nchi tofauti tofauti duniani.
Alisema Tanzania kwa kushirikiana
na Shirika la kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) ilihakikisha kuwa
zaidi ya asilimia 98 ya watoto kutoka DRC na asilimia 79 kutoka Burundi
waliandikishwa kuanza Elimu hapa nchini.
Kwa Mujibu wa takwimu za UNHCR mwaka
2018 Dk Mpango alieleza kuwa idadi ya wakimbizi imeongezeka karibu mara mbili
kutoka watu Mil. 43.3 mwaka 2009 hadi kufikia watu Mil. 70.8 kwa mwaka 2018.
"Ongezeko hili limechangiwa na sababu mbali mbali ikiwamo Vita, Unyanyasaji, Ukiukwaji wa haki za kibinadamu, Machafuko ya kisiasa ambayo yamesababisha
kuobgezeka kwa wakimbizi nchini," alisema Dk. Mpango.
Aidha wengi wa
wakimbizi hao wanatoka katika nchi tano ambazo Ni Syria, Afghanistan, Sudani ya
kusini Myanmar na Somalia huku nusu ya wakimbizi ni watoto wenye umri wa chibi
ya miaka 18. Dk. Mpango aliwasisitiza Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi, NIDA,
RITA na Ofisi ya Taifa ya Takwimu kuendelea kufanya kazi na Mashirika yanayoshughulikia wakimbizi UNHCR kwa kuweka mifumo imara ya upatikanaji wa takwimu
za kiutawala zitakazo saidia serikali kutoa maamuzi ya haraka.
Pia alisisitiza
kutekeleza maagizo yaliyotolewa na Waziri Mkuu kuwataka TAMISEMI, Wizara ya
Fedha na Ofisi ya Takwimu zihakikishe watakwimu wote walioko katika halmashauri
zote wanaripoti kwa Mtakwimu Mkuu wa serikali. Agizo hilo litasaidia kuboresha
na kuimarisha uzalishaji wa takwimu katika halmashauri zote ili kusimamia
utoaji sahihi wa takwimu nchini.
" Napenda kutoa wito kwa halmashauri zote
nchini kuwa takwimu zitakazotumika ni lazima zihakikiwe na Mtakwimu wa
halmashauri ambaye atapata maelekezo yakitaalam kutoka kwamtakwimu Mkuu wa
serikali," alisema Dk.Mpango.
Naye Mtakwimu Mkuu wa Serikali Ofisi ya
Taifa ya Takwimu (NBS), Dk. Albina Chuwa alisema tatizo kubwa linalowakabiri watakwimu
ni kuchagua namna bora ya kupelekea taarifa za takwimu kwa watumiaji kwa njia
nyepesi. Alisema changamoto hiyo aipo Tanzania pekee bali kwa nchi zote duniani
ambapo imebainishwa katika mkutano wa kamisheni ya umoja wa mataifa ya Takwimu
ya mwaka 2013 kuwa tarehe 20 Octoba ya kila baada ya miaka mitano utakuwa ni
siku ya Takwimu duniani.
"Lengo ni kuhamasisha Matumizi mazuri ya Takwimu
katika kutoa maamuzi pamoja na kufuatilia ajenda ya dunia"alisema Dkt.
Chuwa Amewataka Wadau mbali mbali wa Maendeleo kuendelea kudumisha amani na
Ushirikiano ili kujenga uchumi wa viwanda na kufikia malengo endelevu ya uchumi
wa kati.
No comments:
Post a Comment