HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 28, 2019

MOTO WA MABUA UNAVYOTESEKA NA ROHO YA AUSSEMS MSIMBAZI

Na John Marwa

HAKUNA hadithi isiyokuwa na mwisho japo kila hadithi ina muendelezo wake. Ni kama ambavyo wanasayansi hufanya ugunduzi na ufumbuzi wa mambo mapya ambayo yamekuwa yakiendelezwa vizazi na vizazi kila mawio na machweo ya jua. 

Tukiwa hatujaisahau hadithi ya Masoud Djuma na Omogi, tukahadithiwa ya Amunike na nyinge lukuki masiku ya hapo nyuma, imekuja ya Zahera kama kiungua kinywa, maana zilizotangulia zilikuwa kama ndoto. 

Moyo unaukataaa mwili na akili hautaki kusikia wala kuambiwa hautaki hata kupata pumziko la huba kutoka kwa mziwanda aliyeufikisha katikati ya safari ya nchi ya ahadi. 

Tunapoongelea soka la Bongo wakati huu moyo wa soka la Bongo ni wekundu wa Msimbazi Simba SC, hakuna mjadala juu ya hili katika kila nyanja wao wanabaki kileleni. 

Simba wanaukataa ukubwa walioutaka na kuuwaza miongo na miongo, wanataka maisha yale ya sare sare maua, asiyejua Kuchagua kabila lake.... 

Baada ya mvumo mzito uliofanywa mwepesi ndani ya ngoma ya masikio ya wenye kiu ya haki kuwa ni ngonjera za ombaomba leo kiti cha moto anakikalia Profesa Patrick Aussems kujibu kwa nini Midomo ya Chama imekuwa na ushikaji na machupa ya wazungu. 

Kwa nini akili ya Chama imebebwa na upepo wa kisulisuli wa viuno vya Dada zetu wasio haya majumbani kwetu!? 

Kwanini Mkude anaenda mazoezini akiwa amelewa, na vipi kile chumba chake alichokodisha kwenye nyumba moja ya wageni pale Sinza !!!?

Vipi kuhusu kiburi cha Nyoni kwa Uongozi au ustaa wa Gadiel dhidi ya kivuli cha Shabalala!? 

Ushikaji wake na Mkude na Chama leo unamrejesha kule uliko ukoo wake na anakoishi mwanetu Samagoal.
Kinachomhukumu Aussems Simba ni nini? Kuwa ni mtovu wa nidhamu kuliko Mkude na Chama au kwa sababu ya misimamo yake kwa timu kutokaa kambi!? 

Simba inajinasibu klabu kubwa ,inajiendesha kiuledi na kisasa, usasa ni wakuwa na wachezaji wasio jitambua kujua kazi zao na wajibu wao kwa mwajiri wao???! 

Hapa kuna 20% wachezaji wa viongozi hawaguswi hawasemwi hata kama wananuka kwao wananukia hii ndo klabu kubwa. 

Bahati mbaya baadhi ya wanahabari nao wameingia kwenye mkumbo wa kulinda uozo wa Uongozi wa Simba walichokifanya kwenye usajili kinyume na matakwa ya Aussems.
Kakaangu Charles Abel anasema "Ni simba ambao wamemuajiri uchebe na ni simba ambayo inamtimua uchebe.

Shamba ni la bwana heri. Mbuzi ni wa bwana heri na hao mbuzi wamekula mazao yaliyopp shambani kwa bwana heri"

Acha tuendelee na soka letu kivyetu vyetu, Je Simba kama wako Smart, Uchebe sio mwanasaikolojia wa kuwajenga wachezaji wake kiakili waweze kujitambau, kiasi cha kuwa mchezaji wa klabu kama ya Simba, mchezaji anapaswa kujitunza sio kutunzwa.

Leo tutabeba mavuvuzela kuimba Uchebe aondoke kisa kagoma kumuweka Mkude kambini kwenda kuchezaji dhidi ya Biashara United??

Utasikia kuna mengi ndani bwana mdogo, hizi kauli huwa za kishujaa sana lakini nami nawaambia kuna mengi ya hovyo yanafanywa, yamekuwa manukato kwa wenye uroho na njaa za kujitakia.


Na John Marwa
#unstoppable

No comments:

Post a Comment

Pages