Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Mandeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza na viongozi wilaya ya
Kilombero pamoja na watendaji wa sekta ya ardhi katika halmashauri ya wilaya ya
Kilombero na Mji wa Ifakara wakati wa ziara yake ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya
ardhi mkoani Morogoro jana. Aliyevaa miwani ni Mkuu wa Wilaya ya Kilombero
James Ihunyo.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Mandeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiangalia baadhi ya wadaiwa wa kodi ya
pango la ardhi kupitia mfumo wa ukusanyaji kodi ya ardhi kwa njia ya
kielektroni katika ofisi za ardhi za halmashauri ya Mji wa Ifakara jana. Wa
pili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kilombero James Ihunyo. (PICHA NA WIZARA YA ARDHI).
Na Munir Shemweta,
WANMM KILOMBERO
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt
Angeline Mabula ameiagiza halmashauri ya wilaya ya Kilombero mkoa wa Morogoro
kuzifuatilia taasisi za serikali zinazodaiwa kodi ya pango la ardhi kwenye
halmashauri hiyo zaidi ya bilioni 1.9 ili ziweze kulipa deni hilo.
Dkt Mabula alitoa agizo hilo jana alipokutana na uongozi wa
wilaya ya Kilombero pamoja na watendaji wa sekta ya ardhi katika halmashauri za
wilaya ya Kilombero na ile ya Mji wa Ifakara
wakati wa ziara yake ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi katika
mkoa wa Morogoro.
Agizo hilo la Dkt Mabula linafuatia kuelezwa na Mkurugenzi wa
Halmashauri ya wilaya ya Kilombero Injinia Stephano Kaliwa kuwa miongoni mwa
wadaiwa sugu wa kodi ya pango la ardhi katika halmashauri yake ni taasisi za
serikali zinazodaiwa zaidi ya bilioni 1.9.
Alizitaja taasisi hizo kuwa ni Shirika la Umeme Tanzania
(TANESCO) linalodaiwa zaidi ya bilioni 1.7 katika maeneo yake inayomiliki ya
Kidatu shilingi 1,007,452.00, Kihansi 996,957,750.00 pamoja na Mlimba
29,826,650.00. Pia taasisi ya The Trustees of TANAPA nayo inadaiwa jumla ya
shilingi milioni 12,819,550.00.
Hata
hivyo, Afisa Mipango Miji wa Halmashauri ya Wilaya ya
Kilombero Remigi Lipiki alimueleza Naibu Waziri Mabula kuwa, TANESCO
imetaka kufanyika uhakiki kwanza wa deni lake kwa madai kuwa baadhi ya
maeneo inayomiliki yalishachukuliwa na taasisi nyingine na kutolea
mfano wa eneo la Kidatu.
Dkt Mabula alisema, halmashauri ya wilaya ya Kilombero lazima
ihakikishe inazifuatilia taasisi hizo ili ziweze kulipa madeni ya kodi ya ardhi
kwa kuwa taasisi hizo zimekuwa zikitenga fedha kwa ajili ya malipo ya huduma
mbalimbali ikiwemo kodi hiyo ya pango la ardhi.
‘’Taasisi zinashindwa kulipa madeni na hazijachukuliwa hatua,
haiwezekani deni lifikie zaidi ya bilioni moja, fuatilieni suala hili na mchukue
hatua za kisheria.’’
alisema Dkt Mabula
Hata hivyo, Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kilombero
alieleza changamoto kubwa inayoikabili halmashauri yake kuwa ni ukusanyaji kodi
ya pango la ardhi kwa baadhi ya wawekezaji wa Mashamba kutokana na kutokamilika
taratibu za uhaulishaji mashamba hayo ambayo wamiliki wake hawana nyaraka.
Aliataja baadhi ya wamiliki wa mashamba hayo kuwa, ni Kampuni ya Mufindi Paper Mills yenye hekta
10,000 , Green Resource Limited hekta 25,000, Hiragro Ltd hekta 1500 na Sygen
yenye ekari 30,000.
Kwa mujibu wa Kaliwa, kutokana na kutokamilika mchakato wa
uhaulishaji wa mashamba hayo kumekuwa na upotevu wa makusanyo ya kodi ya jumla ya
shilingi 132,865,031.00 kila mwaka.
No comments:
Post a Comment