Waziri Mkuu Kasim Majaliwa akitambulishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (katikati), kwa Ofisa Biashara Mkuu wa benki hiyo, Dk. Joseph Witts, wakati alipowasili kufungua Kongamano la Uwezeshaji kwa Wakandarasi na Wazabuni Kanda ya Kusini lililofanyika mjini Mtwara. Waziri Mkuu aliwahamasisha Wakandarasi na Wazabuni kuchangamkia fursa ya mikopo bila dhamana inayotolewa na CRDB. (Na Mpiga Picha Wetu).
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela akihutubia wakati wa Kongamano la Uwezeshaji kwa Wakandarasi na Wazabuni Kanda ya Kusini.
David Jere, Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakandarasi (CRDB) akihutubia wakati wa Kongamano la Uwezeshaji kwa Wakandarasi na Wazabuni Kanda ya Kusini.
Katibu tawala wa mkoa wa Mtwara, Alfayo Kidata (wakwanza kushoto) akiwa na Mbunge wa Mtwara vijijini, Hawa Ghasi wakiwa katika Kongamano la Uwezeshaji kwa Wakandarasi na Wazabuni Kanda ya Kusini.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela wakati wa Kongamano la Uwezeshaji kwa Wakandarasi na Wazabuni Kanda ya Kusini.
Na Mwandishi Wetu
Mtwara, 18 Novemba
2019. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka wakandarasi
kutumia mabenki kuchukua mikopo ili kuwawezesha kukamilisha miradi yao kwa
wakati na kuacha kutegemea malipo ya awali ya mradi husika ambazo zimekuwa
zikichelewa na kufanya miradi kutokamilika kwa wakati.
Ameyasema hayo leo wakati akizungumza katika kongamano lililo andaliwa
na Benki ya CRDB kwa ajili ya wakandarasi ,wazabuni na wafanyabishara wa
mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma, lilifanyika katika ukumbi wa Benki Kuu, mjini
Mtwara. Kongamano hilo lililenga kuwapatia washiriki hao elimu juu ya matumizi
sahihi ya fedha za mikopo wanazozichukua kwa ajili ya kutekeleza miradi
mbalimbali.
Waziri Mkuu Majaliwa amesema kuwa, wakandarasi ni sekta muhimu sana
katika ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo hapa nchini hivyo wanapaswa
kuboresha utendaji kazi wao kwa kuchukua mikopo toka taasisi za fedha na
mabenki. Ameongeza kuwa, changamoto kubwa inayowakabili wakandarasi wengi ni
ukosefu wa mitaji kwa ajili ya kuendesha miradi mbalimbali ambapo changamoto
hiyo huchangia kutomalizika kwa miradi kwa wakati.
“Benki ya CRDB imewaletea fursa mlangoni, itumieni
vilivyo, changamkieni fursa hizo ili muweze
kukuza biashara zenu na kupata faida zaidi, kuongeza ajira kwa vijana wetu na
hatimaye kulipa kodi stahiki za serikali. Ni
matarajio yangu kuwa, baada ya kongamano hili tutaona utofauti mkubwa kutoka
kwa wakandarasi na halmashauri, ambao wamekuwa wakipitia changamoto katika
kukamilisha miradi yao, kutokana na suala la mapato na ukwasi” alisema Waziri
Mkuu.
Mheshimiwa Majaliwa pia alipongeza benki ya CRDB kwa kuwa mstari wa
mbele katika kuunga mkono juhudi za serikali katika ujenzi wa miondombinu
mbalimbali ambayo itasadia kuchochea ukuaji wa uchumi. Alisema “Benki ya CRDB imekuwa ina fadhili miradi mbalimbali ya kimkakati
inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano katika jitihda zake za kuifanya
Tanzania kuwa nchi ya viwanda.
Tunatambua na kuthamini sana ushikiri wa Benki
ya CRDB
katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo kama vile mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR),
mradi wa umeme wa maji katika bonde la Rufiji (Nyerere Hydro Power Project) na
ule wa kusambaza nishati ya umeme vijijini yaani REA. Kipekee kabisa
niwapongeze tena Benki ya CRDB kwa utayari wenu, ambao mmekuwa mkiuonesha
katika kuisaidia Serikali, hususan katika utekelezaji wa miradii mikubwa ya
kimkakati”. alisema.
Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa
Benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela amesema kuwa,kongamano hili ni fursa pekee ya
kuwakutanisha wakandarasi, wazabuni na
wafanyabisahra ili kuwajengea uwezo na
kuwajulisha fursa mbalimbali za kifedha zilizomo ndani ya benki ya CRDB, na namna
ya kuzitumia fursa hizo ili kukuza miradi na biashara zao.
“Tuna
bidhaa nyingi mahususi kwa ajili ya kundi hili la wateja ikiwamo: Purchase
Order Financing, Contract financing, and Invoice Discounting ambazo hazihitaji
dhamana yoyote kutoka kwa Mkandarasi au mzabuni pindi anapotaka kukopa. Zaidi
ya hilo, Benki pia hutoa mikopo kwa ajili ya upatikanaji wa vifaa vya ujenzi,
magari, mashine, Mabasi na huduma nyingine
kama vile dhamana ya malipo ya awali (Advance Payment Guarantee), dhamana ya
Utekelezaji wa Miradi (Performance Guarantee), Barua za Mikopo (Letters of
Credit), Huduma za Bima na pia tunatoa mikopo ya muda mfupi kama mitaji ya kufanyia kazi” alisema.
Naye mmoja wa Wakandarasi Henry Shimo ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya Chibeshi
constructions Ltd , amesema kuwa, swala
zima la uwezeshwaji wa mikopo hiyo litawasaidia kwa kiasi kikubwa sana
wakandarasi hao kumaliza miradi yao kwa wakati kwani changamoto kubwa ilikuwa
ni mitaji kwa ajili ya kuendeleza miradi yao. Amesema kuwa, kinachotakiwa kikubwa ni uaminifu wa wakandarasi katika
kujua fedha wanayopewa inahitaji kufanyiwa kazi na kurudishwa kwa wakati.
No comments:
Post a Comment