Baba wa Uzao wa Kanisa Halisi la MUNGU BABA akiwahutubia waumini wa Kanisa hilo (hawapo pichani) hivi karibuni.
Waumini wa Kanisa Halisi la MUNGUN BABA wakiwa katika moja ya Ibada za Kanisa hilo.
Na Mwandishi Wetu, Arusha
KANISA Halisi la MUNGU BABA limesema Afrika ni Bara
lenye nuru kubwa na si sehemu yenye giza
kama linavyosemwa.
Kauli hiyo
imekuja baada ya kuwepo kwa miaka mingi ya waafrika kuaminishwa kuwa Bara lao
ni sehemu ya giza na hakuna nuru yoyote inayopatikana ili hali inarasilimali za
kutosha ikiwemo madini,mito,mabwawa,bahari, misitu wakiwemo viumbe mbalimbali wa
baharini na wanyamapori.
Akizungumza
na mamia ya wananchi na waumini wa
Kanisa hilo katika Mji Mdogo wa Namanga wilayani Longido Mkoa wa Arusha, Baba
wa Uzao wa Kanisa hilo amesema Afrika ni Bara la nuru na si la giza
Amesema kwa
kuwa utendaji wa nafsi ambao ulikuwa unaruhusu watu kuibiana vipawa,
karama,talanta na viwekezo sasa umefika kwenye ukomo.
Amesema
hicho ndicho kilikuwa kilele cha ubaya wa kila aina kwa kuonea na kumzonga
mwingine na hatimaye kumwangamiza kwa sababu tu ya vitu vizuri alivyopewa na
MUNGU BABA.
Amesema kwa
Tanzania heri imeanza kuonekana kwa
maana ya kuishi unachosema, kuishi ya moyoni siyo ya mdomoni na Moyo wako kusomeka
usoni kwako.
“Wengi
hawajajua kwa nini Rais Dk. John Magufuli amefanikiwa ndani ya muda mfupi na kwa nini
anapendwa na MUNGU BABA, ni kwa kuwa anaishi kile anachosema na huko ndiko
kuishi Moyo”amesema Baba wa Uzao
Amefafanua kuwa
sauti mpya iliyoanzia Tanzania, Afrika, kwenda katika Mataifa mengine, ndicho
kitu kikubwa ambacho kinasababisha sasa Afrika iwe nuru siyo giza kama
linavyosemwa.
Amesema matatizo
yote ya Afrika, asilaumiwe yeyote, bali kulikiuwa na vitu vitatu ikiwemo Vita
na Ufunuo ambayo ilikuwa inawaingia wale wote ambao wanaonekana ni wakorofi.
“Giza, kwa
maana ya umasikini na ubaya tunaoona katika Bara la Afrika, narudia kusema
kuwa, ilikuwa ni hii miduara mitatu.
“Hata yule
mwandishi wa Kitabu Kikubwa, aliyekiweka kwenye google, kuwa Afrika ni Bara la
giza, aliingiwa na ufunuo,nyoka na vita, maana hizo ndizo nafsi zilizokuwa
zinajua kuwa Afrika ni nuru, wakageuza kibao kuwa ni giza”amesema Baba wa Uzao
No comments:
Post a Comment