HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 07, 2019

MADAKTARI BINGWA WA MIFUPA WA WATOTO WAONGEZEKA MOI

Rais wa Uganda Yoweri Museveni  (katikati), akimpongeza Daktari Bingwa wa Mifupa wa Watoto kutoka Taasisi ya Tiba na Mifupa (MOI), Bernad Luziba, katika hafla iliyofanyika nchini Uganda.


Na Asha Mwakyonde

DAKTARI  Bingwa wa  Mifupa wa Watoto kutoka Taasisi ya Tiba na Mifupa (MOI), Bernad Luziba, amehitimu mafunzo maalum ya Upasuaji wa Mifupa ya Watoto ya COSECSA ambapo amekuwa mwanafunzi bora wa mafunzo wa mwaka 2019, katika hafla iliyofanyika Kampla nchini Uganda.

Akizungumza na mwandishi wetu jijini Dar es Salaam Disemba 6, 2019 Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa Taasisi  ya MOI, Patrick Mvungi, amesema kuwa Dk. Luziba ameongeza idadi ya madaktari bingwa wa mifupa wa watoto katika taasisi hiyo.

Mkuu huyo wa kitengo hicho amesema Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuaa Rais wa Uganda Yoweri Museveni ambayo  ilifanyika Disemba 4 mwaka huu ambapo madaktari bingwa wamehitimu  waliokua mafunzoni.

"Taasisi ya MOI ni moja ya kituo cha kufundishia madaktari bingwa wa upasuaji COSECSA," amesema Mvungi.

Ameongeza kuwa ni  heshma kubwa kwa taasisi na Nchi kuongeza idadi ya madaktari bingwa ambao bado hawatoshelezi,

No comments:

Post a Comment

Pages