Viongozi wa Chadema wakiwa katika kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo.
Na Janeth Jovin
MBUNGE wa Iringa, Peter
Msigwa (Chadema) ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa maadili
ya Uchaguzi hayaruhusu kutolewa kwa hotuba za viashiria vya chuki na
uvunjifu wa amani wakati wa Kampeni za Uchaguzi.
Msigwa
ambaye anayekabiliwa na kesi ya uchochezi pamoja na vigogo wengine nane
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), alieleza hayo jana
katika Mahakamani hapo wakati akitoa utetezi wake mbele ya Hakimu Mkazi
Mkuu Thomas Simba.
Akihojiwa na wakili wa
serikali Mkuu Faraja Nchimbi, Msigwa alidà i kuwa maadili hayo pia
yanazuia watu kuingia katika vituo vya kupigia kura wakiwa na siraha.
Msigwa
alidai, aliudhuria mkutano wa kufunga Kampeni ya uchaguzi wa marudio
jimbo la Kinondoni Februari 16 mwaka jana na kwamba baadhi ya viongozi
na wabunge waliotoa hotuba hawapo mahakamani.
"Mimi binafsi nilihutubia wananchi, sikumbuki kama Mdee alihutubia, Mbowe pia alihutubia" alidai Msingwa.
Mshtakiwa
huyo alidai washtakiwa wenziwe ni miongoni mwa Viongozi wa chadema
walioudhulia mkutano huo na kuna baadhi ya wabunge waliohutubia
katika mkutano huo lakini hawapo mahakamani.
Alitaja baadhi ya wabunge hao ni Frank Mwakajoka, Ernest Silinde, Said Kubenea, Mwita Waitara na John Heche.
Alidai,anapokuwa
katika mkutano wa hadhara lengo hadhira imuelewe,hivyo lazima
azungumze lugha wanayoielewa kwani wanahutubia watu wa biwango tofauti
vya uwelewa.
Katika hatua nyingine alidai,
hajawahi kufanya kazi Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ama ofisi ya
Msimamizi wa Uchaguzi na kwamba Uchaguzi Mkuu husimamiwa na tume hiyo.
Washitakiwa
wengine ni katika kesi hiyo ni Mbunge wa Iringa mjini, Peter Msigwa,
Naibu Katibu Mkuu Taifa, Zanzibar, Salum Mwalimu, Mbunge wa Kibamba,
John Mnyika, Katibu Mkuu Taifa, Vicent Mashinji , mbunge wa Bunda Ester
Bulaya na Mbunge wa Kawe Halima Mdee.
Wengine ni Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche,
Dokta Vicent Mashinji ambaye ni ,Katibu Mkuu taifà wa chama hicho na Ester Matiko.
Washitakiwa
wanakabiliwa na mashitaka 13 likiwemo la kula njama, ambapo wote
wanadaiwa kuwa, Februari 1 na 16, mwaka jana, Dar es Salaam walikuĺa
njama ya kutenda kosa la kufanya mkusanyiko usio halali na kukiuka tamko
kutawanyika.
No comments:
Post a Comment