HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 05, 2019

RC KAGERA AJIVUNIA MIRADI YA MAENDELEO

 Mkuu wa Mkoa wa Kagera akishiriki usafi katika soko kuu la Bukoba kama sehemu ya wiki ya maadhimisho ya Miaka 58 ya Uhuru wa Tanganyika.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Gaguti, akizungumza na wananchi mkoani Kagera baada ya kushiriki kufanya usafi katika soko kuu la Bukoba kama sehemu ya wiki ya maadhimisho ya Miaka 58 ya Uhuru.


Na Lydia Lugakila, Bukoba


Mkuu wa mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti ametumia wiki ya maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru kwa kuwaelezea wananchi mambo makubwa yaliyofanywa na Rais Dk. John Magufuli ndani ya miaka minne na kuwanufaisha wananchi mkoani humo.


Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia, Marco Elisha Gaguti, ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wafanyabiashara wadogo na wakubwa katika soko la kuu la Bukoba kama sehemu maalumya kuwaelezea wananchi kazi kubwa zilizofanywa na Rais Magufuli katika awamu ya tano iliyopelekea mkoa huo kunufaika na huduma mbalimbali ikiwemo utalii, elimu, kilimo, sekta ya afya, miundombinu ikiwa ni pamoja na ujenzi na ukarabati wa meli mpya unaoendelea.
 
Amesema mkoa huo ni sehemu mojawapo ya wanufaika wakubwa wa kazi za Dk. Magufuli kwani tangu miaka minne ya awamu ya tano ya uongozi wa Rais Magufuli miradi mbalimbali imekamilika na kuanza kutumika.

Akitaja miradi hiyo amesema ni pamoja ujenzi wa shule kongwe ya sekondari Bukoba ambapo zaidi ya shilingi bilioni 1.4 zimetumika na mkoa mzima kupokea shilingi bilioni 3.2 kwa ajili ya ukarabati wa shule kongwe, na shilingi bilioni 1.2 kwa ajili ya shule za msingi, ujenzi wa chuo kipya cha veta chenye thamani ya shilingi bilioni 20, na kuwa katika suala ya afya mkoa huo umefanikiwa kupata hospitali mpya 3 zilizojengwa wilayani Kyerwa, karagwe, na Halmashauri ya wilaya ya Bukoba ambapo tayari shilingi bilioni 1.5 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa hosptali mpya wilayani Biharamulo mkoani humo.

Amewataka wananchi hao kila mmoja kwa nafasi yake kupiga vita vitendo vyote vya hujuma vya kuihujumu nchi badala yake waendelee kuwajibika katika kufanya kazi, kuwa wabunifu sambamba na kuitetea na kuilinda amani ya nchi na kujenga moyo wa shukrani yanapotendeka mema.


‘’katika kuona hiyo haitoshi katika kipindi cha miaka minne hii tumepata vituo vya afya 14 vyenyee thamani ya shilingi bilioni 5.9 ongezeko la vituo vya dawa muhimu kwa zaidi ya mara nane ikilinganishwa na huko nyuma ambapo miaka ya nyuma ilikuwa inapatikana shilingi milioni 800 kwa mwaka na kuwa kwa awamu hii zinapatikana shilingi bilioni 5.4 kwa ajili ya madawa muhimu.’’alisema Brigedia Gaguti.


Aliongeza kuwa mwishoni mwa 2020 kutakuwepo na meli mpya kubwa zaidi ya MV Victoria itakayotumika kwa ajili ya mizigo na abiria itakayokuwa na safari katika nchi za Portugal, Uganda, na Kenya.

Aidha amewataka wananchi hao kuwa sehemu ya tija na ongezeko la thamani la maisha yao binafsi na kwa uchumi mkubwa taifa la Tanzania.


Ameongeza kuwa ni muda sasa wakati inapoadhimishwa miaka 58 ya Uhuru kasi iongezwe katika kufanya kazi kwa kujituma zaidi na kutoa mchango mikubwa katika maendeleo ya taifa la Tanzania.


Hata hivyo Mkuu wa mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti Ametumia wiki ya maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru kufanya shughuli za kijamii ikiwemo usafi wa mazingira na uchangiaji Damu Katika Hospitali ya rufaa ya mkoa huo ili kunusuru watanzania Wenye uhitaji wa Damu kumshukuru rais kwa shughuli mbalimbali za kimaendeleo zilizofanyika katika mkoa huo.

No comments:

Post a Comment

Pages