HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 02, 2019

TAASISI YA SARATANI OCEAN ROAD YAOKOA BILIONI 10.4

 Mkurugenzi wa Taasisi ya Saratani ya OceanRoad, Dk. Julius Mwaiselage, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani).


Na Asha Mwakyonde

TAASISI ya Saratani ya Ocean Road (ORCI), imejivunia mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa John Magufuli  kwa kuokoa Sh. Bilioni 10.4 kwa kutosafirisha wagonjwa 208 kutibiwa nje ya nchi pamoja na kuongeza idadi ya wagonjwa waliohudumiwa katika taasisi hiyo.

Pia Mkoa wa Dar es Salaam unangoza kuwa na wagonjwa wenye saratani ya matiti kutokana na kuwa na watu wengi huku wengine wakiwa na uzito mkubwa, kutonyonyesha watoto wao kwa kipindi cha miaka miwili.

Haya yamesemwa  jijini Dar es Salaam leo Disemba 2, 2919 na  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Dk. Julius Mwaiselage wakati akizungumzia mafanikio waliyopata katika miaka minne ya Rais  Magufuli.

Amesema taasisi hiyo imeongeza mapato kutoka sh. milioni 569.9 mwaka 2014/2015 hadi kufikia sh. Bilioni 14.77 mwaka 2018/2019 huku bajeti ya dawa ikipanda kutoka sh. milioni 790 mwaka 2015/2016 hadi sh. bilioni 10 mwaka 2018/2019.

Amesema  taasisi hiyo imekuwa ikipokea wagonjwa kutoka nchi jirani za Kenya, Comoro, Malawi, Msumbiji, Zimbabwe, Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo pamoja na Burundi jambo lililosababisha kukuza mapato ya taasisi.

Mkurugenzi huyovameeleza kuwa  mwaka 2015 walikuwa wakipata wagonjwa wa nje ya nchi 30 hadi 35 lakini kutokana na kuongezeka kwa vifaa tiba, kusini mwa jangwa la Sahara wamefikia wagonjwa 304 mwaka 2019.

 "Serikali imetoa sh bilioni 9.5 kununua mashine ya kisasa ya tiba ya saratani ya mionzi ya Linear Accelerator pamoja na CT Simulator, " amesema.

Amesema mashine hizo  zilianza kutoa huduma za uchunguzi na tiba Septemba, 2018 ambapo juma ya wagonjwa 1,141 wameshatibiwa, kati ya hao wagonwa 208 wangepelekwa nje ya nchi kama mashine hizi zisingekuwepo na hivyo serikali imeweza kuokoa sh bilioni 10.4.

Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa  gharama za mgonjwa mmoja kutibiwa nje ya nchi ingegharimu sh. milioni 50 hadi sh. milioni 75 ambapo pia mashine hizo zimepunguza muda wa wagonjwa kusubiri tiba mionzi kutoka wiki 6 hadi wiki 2.

Amefafanua kuwa mashine ya CT simulator imesaidia kuanzisha huduma za CT Scan ambapo hadi kufikia Septemba, 2019 wagonjwa 1,430 walikuwa wamepata kipimo cha CT Scan na kupunguza usumbufu kwa wagonjwa kupata huduma hiyo nje ya taasisi.

Amesema upatikanaji wa dawa kwenye taasisi hiyo umefikia asilimia 95 mwaka 208/2019 ambapo kwa wagonjwa wa saratani zinazoongoza kama saratani ya mlango wa kizazi, matiti, Kaposi Sarcoma, tezi dume, njia ya chakula kooni, damu, matezi, ngozi na kibofu cha mkojo hutolewa kwa asilimia 100.

Dk. Mwaiselage ameeleza kuwa juhudi za kununua mashine mpya za tiba mionzi na kuimarisha upatikanaji wa dawa, umepunguza rufaa za wagonjwa kutoka 164 mwaka 2015 hadi wagonjwa 14 mwaka 2019.

“Wagonjwa wengi walikuwa wanakwenda nje kwa ajili ya upasuaji na tiba mionzi ya kisasa na tiba kemia, kwasasa huduma zote hizi zinapatikana nchini kwa kushirikiana na Hospitali ya taifa Muhimbili katika upasuaji,”amesema.

“Upatikanaji wa kipimo cha PET/CT Scan utapunguza gharama zitokanazo na kupeleka wagonjwa nje ya nchi, serikali itaokoa sh bilioni 5 kila mwaka,”alisema.


Amezungumzia Mkoa Dar es Salaam Saratani ya Matiti inaongoza kuwa na wagonjwa wengi ambayo husababishwa na vyanzo vingi kama uzito mkubwa, uzazi watu hawataki kuzaa sana na kunyonyesha huchochea visababishi vya saratani ya matiti,”alisema.

Amesema ugonjwa wa saratani hutofautiana idadi kila mkoa kutokana na namna ya maisha ambayo watu huishi huku akiitaja mikoa ya Kanda ya ziwa kuongoza kwa saratani ya kibofu cha mkojo huku Mbeya ikiwa na saratani ya mlango wa Kizazi.

No comments:

Post a Comment

Pages