HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 02, 2019

BOTI YA UVUVI YAZINDULIWA ZANZIBAR

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akielekea katika sehemu ya maonesho ya Bidhaa za Baharini wakati wa Uzinduzi wa Boti Mpya ya Kampuni ya Uvuvi Zanzibar(ZAFICO) katika viwanja vya Hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar, (kulia kwa Rais) Mkurugenzi wa Uvuvi Zanzibar.Ndg.Mussa Aboud Jumbe na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Uvuvi Zanzibar(ZAFICO)Ndg, Zahro Kassim Mohammed.(Picha na Ikulu).
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Kiongozi wa Kikundi cha Wajasiriamali wa Kuanika madaga cha Shina Group cha Pemba.Ndg.Dadi Hamad Dadi, akipata maelezo ya ukuashuji wa Dagaa, wakati akitembelea maonesho hayo baada ya kuzindua Boti Mpya ya Sehewa ya Kampuni ya Uvuvi Zanzibar.(Picha na Ikulu)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Kiongozi wa Kikundi cha Furahia Wanawake cha Paje Wilaya ya Kusini Unguja.Bi. Kidawa Suleiman Ali, akitowa maelezo ya sabuzi za Mwani na mafuta, wakati akitembelea maonesho hayo, baada ya kuizindua Boti ya Sehewa katika ufukwe wa bahari ya Hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar.(Picha na Ikulu)
Baadhi ya Wananchi na Wajasiriamali wa Vikundi vya Uvuvi Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia hadhara hiyo(hayupo pichani) wakati wa hafla hiyo ya Uzinduzi wa Boti mpya ya Uvuvi ya (ZAFICO).
 Waziri wa Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi Zanzibar.Mhe. Mmanga Mjengo Mjawiri akihutubia wakati wa hafla hiyo ya Uzinduzi wa Boti ya Kampuni ya Uvuvi Zanzibar,(ZAFICO) hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein, akihutua wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Boti ya Uvuvi ya Sehewa ya Kampuni ya Uvuvi Zanzibar(ZAFICO) hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

Pages