Mwandaaji wa tamasha la Moyo wa Ibada, Paul Mwangosi, akizungumza na waandishi wa habari kuelekea tamasha hilo linalotarajiwa kufanyika kesho Desemba 13, 2019 katika viwanja vya Tanganyika Parkers jijini Dar es Salaam.
Mwimbaji wa nyimbo za injili kutoka Kenya, Sarah Mwangi ‘Sarah K’, akizumgumza na waandishi wa habari kuhusu tamasha la Moyo wa Ibada litakalofanyika Desemba 13, 2019 katika viwanja vya Tanganyika Parkers jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Jeremi Kitiku na Mwandaaji wa tamasha hilo, Paul Mwangosi.
Mwimbaji wa nyimbo za injili kutoka Kenya, Sarah Mwangi ‘Sarah K’, akiimba moja ya nyimbo zake wakati wa mkutano na waandishi wa habari jana kuelekea tamasha la Moyo wa Ibada litakalofanyika Desemba 13, 2019 katika viwanja vya Tanganyika Parkers jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande).
Na Mwandishi Wetu
MSIMU
wa pili wa Tamasha la Mkesha wa Usiku wa Moyo wa Ibada utaunguruma kesho
katika Viwanja vya Tanganyika Packers Kawe jijini Dar es Salaam.
Tamasha hilo linaandaliwa na huduma ya Moyo wa Ibada chini ya Mwimbaji wa nyimbo za Injili Paul Mwangosi.
Lengo
Kuu ni kuwakutanisha watanzania kurudisha shukrani kwa Mwenyezi Mungu
na kusema asante kwa ulinzi wa mwaka mzima sabamba na kuliombea Taifa
katika nyanja mbalimbali.
Akizungumza kuelekea Tamasha hilo Paul Mwangosi amesema ni mkesha wa Ibada ya kumsifu , kuabudu na kumshukuru Mungu.
"Tutakutana
hapa kwa ajili ya kumshukuru Mungu kwa kutulinda mwaka mzima, tutaimba
na kusifu sambamba na kupata neno la uzima lakini pia tutapata nafasi ya
kusema neno kwa ajili ya nchi yetu.
"Natamani
kila mmoja awe sehemu ya tamasha hili na sehemu ya ibada hii kama
ambavyo ndugu zetu kutoka kenya wamekuja kujumuika nasi ."amesema
Mwangosi.
"Mwenyezi
Mungu alituumba ili tumuabudu kwani kumuimbia na kumsifu hata wanyama
na mimea inafanya hivyo, ndio maana hatuchukulii kawaida kwa sababu
imepangwa.
"Katika
kumsifu, kumuimbia na kumuabudu Mungu kuna mambo mengi hufunguka kwenye
maisha yetu, huu ni wajibu wetu kusema asante kwa kutuwezesha kuumaliza
mwaka Salama."amesema Sarah Mwangi mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka
Kenya.
Tamasha hilo
linatarajiwa kuanza majira ya saa 3 usiku hadi alfajiri ya kuamkia
Desemba 14. Wahudumu wanaotarajiwa kuhudumu ni pamoja na Mwandaaji Paul
Mwanaidi, Sarah Mwangi (Kenya) na Boaz Danken.
No comments:
Post a Comment